Sehemu Ya (154) : Hali Halisi Ilivyo Kwenye Mahusiano Siku Hizi.. Unaweza Jifunza Kitu Hapa.

Kuna kijana alikua anajua kuwa mke wake anatoka nje ya ndoa basi akamuuliza
mke, mkewe akakataa, akamwambia baba yake akaambiwa na babaake tulia mwanangu ndoa zina mengi! akawa kila siku analalamika kwa babaake, mwisho babaake akamwambia basi ntakusaidia. Itabidi ujifanye unaumwa sana hoi hujiwezi halafu nitakuonyesha jawabu!

Basi kijana akajifanya anaumwa mzee akaitisha kikao cha ndugu wote pande Mbili Mzee akaanza kueleza jamani kijana wetu anaumwa amepata ugonjwa wa utata hospitali zote umeshindikana hivyo tumeenda kwa mganga wa jadi amenipa dawa na ina masharti, inatakiwa atakaye iandaa hii dawa awe mwanamke mwenye ndoa ambaye hajawahi kutoka nje ya ndoa tangu alipoolewa ndo kijana wetu atapona! Kama ametoka nje ya ndoa asiandae dawa hii kwa sababu tukimpa kijana wetu watakufa wote!

Je, kina mama nani ataandaa? Walitoka nje wamama mmoja mmoja hadi mkewe na mamake mzazi wakatoka, akafata mama ake kijana, mashangazi na dada zake, mwisho wakabakia wanaume peke yao! Mzee akamwambia mwanangu umeona hali za ndoa zilivyo? Acha kujisumbua tulia na mkeo nadhani umejionea hali halisi. Cha zaidi omba Mungu sana juu ya ndoa yako! Kijana akazimia!

Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Ili Kupata Posts Zangu Kirahisi Zaidi Kwenye Simu Yako.http://www62.zippyshare.com/d/FvrvpQQg/31722/xxlbongotz.apk
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies 
WhatsApp +255 715 758 021

No comments