Sehemu Ya (160) : Mpenzi Aliyepoteza Ladha Katika Mahusiano Yake.. Utamjuaje??
ktk kila jambo, kauli mbovu na sauti ya juu wakati akiwa anazungumza
na mumewe hivyo ni vitu vya kawaida sana kwake, hana hofu juu ya ndoa yake
yaani si wife material tena.
_Hupenda mabishano kwenye kila kitu, si mtu wa kupokea maagizo kutoka
kwa mumewe na kuyafanyia kazi ipasavyo bila kubishana, anapemda kufanya
argumentation kama mbunge wa viti
maalumu.
_Ni mtu wa kulalamika sana kwenye mazuri na mabaya, si mwepesi
kushukuru kwa chochote kiwe kidogo au kikubwa, kila analotendewa kwake si jema
hana kawaida ya kuridhika.
_Tendo la ndoa kwake ni kama adhabu ya push up, kumpa unyumba mumewe
siku hiyo hadi majirani watajua kuwa leo mume anahitaji mzigo, hawezi kulifanya
jukumu hilo kama wajibu wake ila hadi alizimishwe na mara pengine kumpangia
mumewe ratiba siku za kukutana naye kimwili.
_Hajui kitu bahati mbaya, akili yake inamtuma kila analotendewa
limedhamiriwa, yaani hakuna mistakes kwake, mumewe asikosee kitu.
_Mashindano kwake ni jambo la kawaida sana, mfano: mumewe akiwa busy na
kazi asipomtumia msg au kumpigia basi na yeye hufanya vivyo hivyo.
_Hupenda kumlinganisha mumewe na
wanaume zake waliopita (kumtoa kasoro) na marapengine hujuta kuolewa na mume
alienaye na kuwaona waliokuwa wakimchezea ni bora zaidi ya mumewe.
Inawezakana ikawa ni kweli wanaume ndio wanaongoza kuvuruga ndoa zao.
Ila je ulishawahi kujiuliza kwamba uwenda mwanaume wako anachepuka kutokana na
kero zako.?
Ili ndoa iwe bora inahitaji amani na upendo, utulivu wa nafsi na upole
kwa kila mmoja. Mwenyejukumu la kufanya ndoa iwe bora si mwanaume pekee ila
hata wewe mwanamke pia ni mtu muhimu kuipigania ndoa yako kuwa ktk misingi
imara.
Usipende kuishi kwa mazoea.
Jitathmini Mwanamke.
Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment