Sehemu Ya (94) : Kwenye Mapenzi Kuna Mambo Sio Ya Kulazimisha Kabisa Yasome Hapa.
Usijaribu kulazimisha mambo. Hauwezi kulazimisha kupenda, hauwezi
kulazimisha attention ya mtu kwako. Hauwezi kulazimisha jitihada ya mtu.
Hauwezi kulazimisha 'chemistry'. Hauwezi kulazimisha mtu kukuelewa.
Hauwezi kulazimisha uvumilivu wa mtu, na mbaya zaidi hauwezi kulazimisha
uaminifu.
Yale mapenzi yaliyokuwepo mwanzo sasa hayapo tena, lazima kuna sehemu
yamepelekwa na huwezi kulazimisha kuyarudisha tena. Unazidi kutengeneza hali
mbaya kwa upande wako ukizidi kulazimisha.
Naam, unalazimisha mambo mengine mabaya yatokee kwako. Unazidi
kumsukuma mbali zaidi na wewe. Unazidi kutengeneza umbali kati yako na yeye
kadiri unavyozidi kulilia penzi.
Hujui hili? Ni kwamba unazidi kumpa sababu za kuto kukujali. Kwanini?
Ni kwa sababu unamuonesha ni jinsi gani anaweza kukutawala hisia zako na
kukuchezea atakavyo 'as long as' anajua unampenda sana.
Unamuonesha ni jinsi gani ulivyochanganyikiwa na uzito wa penzi
ulilonalo juu yake. Naam hiyo ni silaha yake kwako ya 'ku-compromise.'
Tafadhali sana usimfanyie hivyo mtu ambae haoni thamani ya maumivu yako
na zaidi usiufanyie hivyo moyo wako.
Kwa upande wako unaona kama unapigania mahusiano yako ila ukweli ni
kwamba unazidi kuumiza moyo wako, kwa sababu hautofanikiwa kufikia matarajio
yako hivyo kujiumiza zaidi.
Angekupenda usingemlazimisha kuwasiliana na wewe, angekupenda
usingemuomba awe karibu na wewe, angekupenda 'automatically' ungejihisi
kupendwa.
Sasa amekuwa mtu ambae hutakiwi kupoteza muda wako tena. Hivyo acha
kulazimisha penzi ambalo halipo tena na limehama. Kimsingi kuna mambo mengi
mengine ya kufanya ili kujitengeneza kuwa mtu bora (a better you).. was good
memory and the best experience..
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment