Sehemu Ya (151) : My Dear Lovely Sisters.. Kama Upo Kwenye Mahusiano Nna Ushauri Kwa Ajili Yenu Hapa... Unaeza Jifunza Kitu.
Huwezi kuwa unatembea ukiwa unakula barabarani mihogo kwenye gazeti,
kachori kwenye mfuko, chips kwenye foil, au miguu ya kuku na utumbo kwenye
mifuko, alafu ukategemea kuheshimiwa na mwanaume anaejitambua wakati wewe
hujiheshimu, jiheshimu uweshimiwe.
Usipende kuongea kwa makelele kama chiriku au kasuku ukiwa na rafiki
zako alafu ukategemea kupewa siri na mpenzi au mume wako, linda kinywa chako na
uropokaji ili ufaidi kushirikishwa siri za mumeo.
Acha kuchezea afya yako kwa kuboost makalio, matiti manukato kupindukia
sehemu za siri na maeneo mengine kwa kigezo cha kuvutia wanaume, asilimia kubwa
ya watu wanaokufa kwa magonjwa ya saratani ni wanawake, nakupa pole sana wewe
unayefanya hivyo, mwanaume atakupenda jinsi ulivyo acha kumtoa Mungu kasoro kwa
jinsi alivyokuumba na kujiumba mwenyewe. Ridhika na uzuri wa asili kutoka kwa
Mungu, utapendwa tu.
Kupoteza muda wako kwenye mitandao kutafuta umbea huko ni kutothamini
muda wako, mtu anayeshindwa kuthamini muda wake huwa ni ngumu sana kujithamini
yeye binafsi. Fid q anakwambia "thamini huu muda kabla haujageuka histori". Jikite kwenye
mambo yenye tija kwako, panua akili yako kuwaza mambo yenye faida juu ya maisha
yako. Usikubali kuendeshwa na mitandao dada angu.
Usipende kujiingiza kwenye mahusiano mapya mapema kila mnapoachana na watu wako wa awali, some
times yakupasa uupumzishe mwili wako na mikiki mikiki ya wanaume, pumzisha
akili kutafakari aina ya mahusiano unayoitaji. Jipe thamani acha kuendeshwa na
mapenzi.
Kuzaa mtoto mmoja au wawili isikufanye uchuje kiasi kwamba mwenekano
wako wa awali wote unapotea, kutwa nzima unashinda na dira na mavitenge tangu umeamka, eti ukiulizwa nini tatizo
mbona unefubaa hivyo, kisingizio kisiwe kulea. Kuna watu wanawatoto zaidi ya
wanne na bado wana good looking kwann wewe?. Acha kujizeesha ungali binti.
Jiheshimu ueshimike, bila kujipenda hutopendwa bali utachezewa. Wewe ni
wa thamani sana kuliko unavyodhani. Badilika.
Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment