Sehemu Ya (142) : Ladies, Kama Upo Kwenye Mahusiano Na Umegeuzwa "Punching Bag" Nna Ushauri Kwa Ajili Yako Hapa.

Duniani kuna binadamu wa aina mbili wale wa roho mtakatifu na roho mtakabifu
ogopa sana kukutana na mwanamke au mwanaume mwenye tabia za aina mbili yaani kama tetecycline hapa nawazungumzia wale wakati wa uchumba au kwenye girlfriend na boyfriend wanaonyesha kukupenda na kukujali mpaka unasema roho mtakatifu kanishukia nmepata chuguo la moyo wangu unatoa na ushuhuda kabisa kwamba Mungu kakutendea..

kimbembe sasa umevalishwa pete la bati mnasubiria ndoa mweeh vanga linaanza mkipishana maneno kidogo ngumi unakula dharau matusi masimango na manyanyaso ya kila aina hapa sasa unaanza kuomba ushauri nifanyaje nibaki na huyu may weather au nisonge mbele ukifikilia ushazaa nae wazimu party two mmechuma mali wote kuanzia zero mpaka kuwa na nyumba gari viwanja na mashamba maduka ndo usiseme unajipa moyo ntavumilia tabia yake ya kunipiga lol wewe ni bwege tena mtozeni sema Amen..

Mwanaume wa kweli hampigi mwanamke hata siku moja mwanamke sio punching bag tabia hizi walikua nazo watani wangu wakurya saivi wameelimika ndo wanaongoza kwa kupenda wapenzi wao kama wewe mwanaume unajiona una nguvu andaa pambano ulingoni mpigane kwa faida watu washangilie na wewe upate hela dadangu ukikutana na kina matumla wa dizaini hii kimbia mapema.. 


Pete sio kigezo cha wewe kubaki kwenye mahusiano yanayokuumiza jitambue jijali wapo watakaopenda kwa mioyo 70 mrudishie bati lake kabla halijawa kutu fanya maamuzi yatakayokuumiza kwa mda mchache ila utaishi kwa furaha milele fanya maamuzi katika njia iliyotukuka be smart usikubali kulegea dunia huruma haina usiteseke kisa unataka ndoa hizo ni formality tu tuliletewa na wazungu kama tulivoletewa dini

Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Ili Kupata Posts Zangu Kirahisi Zaidi Kwenye Simu Yako.http://www62.zippyshare.com/d/FvrvpQQg/31722/xxlbongotz.apk
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies 
WhatsApp +255 715 758 021

No comments