Sehemu Ya (141) : Tunachotegemea Kukipata Kwenye Mahusiano Mapya.. Tofauti Kabisa Na Tulichopewa Kwenye Mahusiano Ya Zamani.

Mtu fulani anapokubali wewe Huwe mpenzi wake mpya baada ya kupitia penzi
lililo below standards anakua na expectations kubwa na wewe kwamba utamsahaulisha maumivu ya penzi la zamani na utaandika historia mpya kwenye maisha yake na kumpa new experience asahau yaliyopita..

Ukapewa nafasi ya kuandika rasimu mpya ya katiba kwenye moyo wa mtu halafu wewe unafika kwenye bunge la hisia zake na kuanza kucheza cheza utamfanya mtu huyo aanze kukumbuka hata yale mema machache aliyokuwa anapewa kwenye katiba ya Zamani kama huna jipya la kuongeza kwenye moyo wa mtu usiangaike kuupokea moyo wake.

Ni heri abaki na katiba yake chakavu aliyoizoea kuliko wewe katiba mpya usiyeeleweka kama una serikali 1 , 2 au 3 unazoziongoza kwenye Moyo wako. Usimfanye mtu amuone EX wake ana afadhali kuliko wewe mpenzi mpya kwa kufeli kufanya yale aliyotegemea na uliyohaidi wakati ukigombea jimbo lake kama akikubali
.

Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Ili Kupata Posts Zangu Kirahisi Zaidi Kwenye Simu Yako.http://www62.zippyshare.com/d/FvrvpQQg/31722/xxlbongotz.apk
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies 
WhatsApp +255 715 758 021


No comments