Sehemu Ya (140) : Hey Single Ladies, Mambo 10 Ambayo Unatakiwa Uyafahamu..
1. Usiharakishe kutoka nyumbani kwa wazazi wako kwa gia ya kwenda
kuolewa.
2. Usimsubiri mwanaume mpaka aje ndio uanze kuishi. Unaweza kuishi
maisha timilifu hata ukiwa huna mwanaume.
3.Achana na pombe zimewauwa wenzako wengi kwa kisingizio cha kuondoa
stress na wewe unaweza kufa pia.
4. Usiwe mtu wa kuendekeza kuzipokea na kuzijibu namba ngeni za simu
hasa nyakati za usiku.. sio njia sahihi ya kukupatia mpenzi.
5. Tengeneza mazingira ya kuilinda afya. Jitahidi Kunywa maji mengi na
Chakula kwa diet achana na viofa ofa vya bure, vimesha waponza wenzio wengi
mpaka sasa.
6. Vaa vizuri na kiheshima. Watu watavutiwa na wewe ulivyo kabla ya
kuongea nawe.
7.Usitumie sex kama ndio mzani wa mapenzi. Unaweza ukaachika tuu pamoja
na penzi lako taamu.
8. Usiolewe na mtu kwa sababu ya fedha; Utabakia kuwa mtumwa wake .
9. Jiongezee ubora wako, Tafuta kazi, Usiwe mpuuzi ukaamini mwanaume
atatatua matatizo yako yote.
10. Jiheshimu sana kwa kuangalia namna ya uvaaji wa mavazi yako na
mwonekano wako mbele ya jamii…. Usitegemee kuvaa kimini ukutane na mwanaume wa
suti… wewe utampata wa milegezo na kubana pua tu.
Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment