Sehemu Ya (137) : Ladies, Kuwa Mnyenyekevu Na Sio Mpumbavu Panapotakiwa Hekima Na Akili Zitumike.
Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu hata ungekua
umemkosea
nini ukijishusha ukanyenyekea analainika labda hawe na mapepo ndio unyenyekevu
wako hautagusa moyo wake.
Mume hafokewi, mume hagombezwi, mume hafanyiwi jeuri na kiburi, akinuna
na wewe unanuna asipokutafuta na wewe humtafuti, utapoteza ndoa yako. Ni mume
wako wa ndoa unaruhusiwa kumng'ang'ania kama ruba.
Asipokutafuta mtafute, asipoongea na wewe ongea naye wewe.
Hakunaga mke anaambiwaga anajipendekeza kwa mumewe. Kunyenyekea
hakukugeuzi kuwa housegirl na ukapoteza nafasi yako ya kuwa mke bora, ila
kiburi na jeuri ndio vitakufukuza kwenye hicho kiti na hiyo nafasi ya kuwa mke
haraka sana.
Ujeuri weka pembeni! ndivyo wanavyofanya waliodumu kwenye ndoa zao.
NOTE: Kuwa mnyenyekevu sio kuwa mpumbavu. Panapotakiwa hekima na akili
zitumie!
Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment