Sehemu Ya (136) : Soma Hapa Kisa Hiki Cha Kweli Cha Wana Ndoa... Unaweza Jifunza Kitu Kwa Kweli.

TAMAA YA MKE WANGU YAVUNJA NDOA YETU.

Jana jioni nilipata mwaliko nyumbani kwa rafiki yangu mmoja ambae pia ni kapteni wa JWTZ kikosi cha anga (Air Transport Station) hapo Majumba sita.

Baada ya kufika nyumbani kwake maeneo ya huku Kitunda, akanijuza anahitaji nimpe namba ya shemeji yangu flani. Nikataka kujua anaitaka ya nini? Bila kusitasita, akanijuza kwamba anauza nyumba yake iliyopo maeneo ya Kivule ili wagawane malipo na mkewe!!

Nikashtuka sana, zaidi ya nilivyoshanga.....!
Nikamuuliza kivipi ilihali mnaishi pamoja kwa ndoa halali ya kikristo?

Akanijibu  "Tumetengana tangu mwezi November!!".

Hili jibu likanipa kizunguzungu haswaa, yaani zaidi ya kushtuka na kushangaa awali, sasa nikapata kizunguzungu.

Awali nikahisi labda ananitania na kwamba tayari pombe ilikuwa inaanza kufanya brain changes zake (maana hawa wajeda wakilewa hawaishagi kufanya vituko vya kuchekesha) lakini akasisitiza kabisa kwamba hatanii wala hafanyi mzaha bali yupo seriously!!

Nikataka kujua imekuaje hadi kufikia hatua ya kutengana (huku nikihisi labda kutokuonekana kwa mkewe, alikuwa likizo huko kijijini maana mkewe huyo ni mwalimu wa sekondari flani ya kata).

Akaanza kunisimulia sasa.

Kwamba, mapema mwezi Oktoba 2017, alipata job part time na night Support Security Kwa ishu flani za kiintelijensia ya kijeshi na wakamuahidi kumpa Tsh 6M kama malipo kwa ajili ya kazi iyo, na Tsh 250,000 kwa ajili ya allowances za usafiri wa hapa na pale, chakula na vocha.

Baada ya mapatano hayo, akamjuza mkewe kama sehemu ya wajibu wake ili ajue kwamba atakuwa anachelewa kurudi nyumbani kwa sababu akitoka kazini, atakuwa anaenda huko KSS HQ na maeneo kadhaa kwa mujibu wa hitaji la hiyo kazi.

Akanambia kwamba, siku 3 kabla ya kuimaliza hiyo kazi akakaa na mkewe ili wapange jinsi ya kuitumia kwa maendeleo ya familia yao (wana watoto watatu).

Basi bwana, katika mjadala huo, mkewe akataka wafungue saluni kubwa ya kupamba wadada ikiwa na uuzaji wa vipodozi, nguo, viatu na mambo kadhaa ya wadada.

YEYE AKAMPINGA kwa hoja kwamba iyo biashara kwasasa ni ngumu sana na haina faida ya haraka haraka, hivyo ni bora wakaongeze vyumba kwenye nyumba yao nyingine (hii anayotaka kuiuza sasa) kisha waongeze idadi ya wapangaji.
MKEWE NAYE AKAKATAA.

Ikabidi wakubaliane kutokukubaliana na kila mmoja akaondoka na hasira zake.

Siku ambayo alikuwa anapewa malipo yake, akamjuza mkewe ili ajue kwamba atarudi na mapesa ayo 6M.

Baada ya kutoka kule KSS alipopewa yale mapesa, hakuona haja ya kuwa na hofu kwa sababu ya taaluma yake ya uofisa wa jeshi.

Akaziweka kwenye begi dogo la kijeshi la mgongoni kisha akapanda gari yake na kuondoka.
Wakati yupo njiani, dada yake akampigia simu apitie kwake Kinyerezi, akaona apitie tu.

Pale kwa dada yake, wakati wanaongea wakawa wanakunywa pombe (dada yake anamiliki Pub hapo hapo mbele kidogo ya nyumba yake na mumewe), ilipofika saa 4hivi usiku, akajihisi ameanza kulewa, hivyo akamwita dada yake ndani na kumjuza kwamba anazo 6M na anaomba abaki nazo ili hata kama kutatokea mushkeri huko njiani, basi pesa ziwe salama apo kwake.

Akatoa pesa zote na kumkabidhi dada yake, lakini begi akaondoka nalo.

Alipofika nyumbani akamkuta mkewe haeleweki heleweki na kwakuwa alikuwa kalewa, hakujali. Akaingia chumbani na kulala huku lile begi ambalo awali alibebea zile 6M alizoziacha kwa dada yake, likiwa kabatini.

Muda mfupi mkewe akaingia chumbani na kuanza kumpa bia zaidi hadi akalewa ingawa sio sana kabisa kisha uyo mkewe akamjuza kuwa mtoto wao anaumwa (wengine wawili wanasoma primary boarding) hivyo ataenda kulala nae. Akamjibu kilevi levi "OK" lakini baadae kidogo alishangaa, tangu lini huo utaratibu wa kulala na mtoto umeanza na mara kadhaa anaumwa lakini haikuwa hivyo?

Akapuuzia na kuamua kulala. Akazidi kunijuza kwamba, majira ya saa 8 hivi usiku akahisi kuna watu au vitu vinanyata kuelekea chumba kalala (akanisisitizia kwamba hisia za kijeshi zilimjuza ivyo).

Akaisogeza karibu bastora yake na kuchomoa magazini ili asiweze kujeruhi mtu bali aitumie kama tishio kwa uyo anayekuja kwa kunyata. Kisha akabana nyuma ya mlango.

Gafla wakaingia vijana wanne wakiwa na mapanga, na yeye nae gafla akawasha taa na kuwanyooshea Ile bastora ambayo haikuwa na risasi.

Lakini haikuwa kama alivyotarajia, wale vijana wakamvamia na kuanza kumkata kwa panga huku yeye akikinga kwa mikono ili wasimjeruhi kichwani wala usoni, anasema baada ya kama dakika 15 hivi huku kukiwa na purukushani kubwa kiasi cha baadhi ya vitu kuanguka, akafanikiwa kuwadhibiti wawili (anadai aliwapiga nyuma ya shingo na kupoteza fahamu) ila wawili wakakimbia.

Haraka akapiga simu kikosini ili kuomba msaada wa kuwahishwa hospitali.

Gari likaja na wanajeshi kadhaa wakiwemo MP na kuanza kufanya uchunguzi wa awali kisha kuondoka na wale vijana wawili ambao hadi muda huo walikuwa bado wamepoteza fahamu.
Anasema, kitu cha ajabu kabisa ni kwamba mkewe hakushtuka kutoka usingizini wala hakutoa msaada wowote ilihali kulikuwa na pilika pilika kubwa baada ya wanajeshi wenzake kufika hapo kwake (anaishi nyumba yake binafsi).

Wiki 1 baadae akapewa ripoti kwamba mkewe ndiye alikuwa master planner na engineer wa huo mpango.. Akanambia hakushtuka wala kushangaa bali aliunganisha matukio ya siku ya tukio na hali aliyomkuta nayo mkewe, jinsi "alivyokimbia kulala pamoja" na kitendo chake cha kumuongezea bia zaidi ilihali mkewe hapendi yeye anywe pombe kupita kiasi.

Akaomba kikosini hiyo kesi aimalize kifamilia (ingawa wakuu wake walimgomea lakini baadae walimkubalia na kumjuza kuwa hao vijana ni waendesha boda boda hapo hapo Kitunda na waliahidiwa kulipa Tsh 1M kwa kazi hiyo ikiwa na maana wangegawana 250,000 kila mmoja).

Akanambia baada ya kukubaliwa, ndipo alipomjuza mkewe kwamba ndoa imekufa rasmi kama yeye alivyowakodi vijana waje kumuua kisha wampore ile pesa ambayo hata hivyo hakurudi nayo bali aliicha kwa dada yake kwakuwa alikuwa keshaanza kulewa..

Akanambia anataka kuuza iyo nyumba kisha pesa yote ampe huyo mwanamke kwasababu ameshajua kuwa anashida ya pesa na sio ndoa.
****************************************************************
Nimeitafakari sana hii kitu na kuona leo niwasimulie ili angalau tupate picha jinsi roho ya tamaa inavyoweza kuingia hata kwa wanandoa kiasi cha kutaka kuuawana ili mmoja apate pesa.


Nawatakia baraka za Mungu huku tukitafakari kwa pamoja kisa hiki cha kweli kilichomkuta rafiki yangu huyu ambaye kama asingekuwa mwanajeshi, angeshakuwa amekuwa mauti kwa tamaa ya mkewe.

Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Ili Kupata Posts Zangu Kirahisi Zaidi Kwenye Simu Yako.http://www62.zippyshare.com/d/FvrvpQQg/31722/xxlbongotz.apk
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies 
WhatsApp +255 715 758 021

No comments