Sehemu Ya (135) : Baadhi Ya Sifa Za Mpenzi Anayekufaa Katika Maisha Yako.
1.Mpenzi wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji yaani
hana sababu ya
kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada.
2. Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa
na wewe kwa hali zote mbili .
3. Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema,
hatojali umeongea baya au zuri
4.Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha. Hatakuwa mtu wa kuvizia
vizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha.
5. Mpenzi wa kweli atakuheshimu na hatopenda kuwa kikwazo cha maisha
yako, atakulinda daima.
6. Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo
fulani (pesa au mali)
7. Mpenzi wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama
rafiki au mpenzi mbele ya wengine, hafichi hisia zake mbele za watu, atakutetea
na kukufanya wa kwanza.
8. Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda
kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli na mwaminifu.
9.Mpenzi wa kweli ni yule anayejiamini, asiyeyumba katika maamuzi hata
kama atalazimika kufanya maamuzi magumu .
10.Atakuwa tayari kuvumilia, hatakuwa mwepesi wa hasira wala kutumia
lugha chafu na ubabe.
Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment