Sehemu Ya (132) : Saa Chache Kabla Ya Kufunga Ndoa.. Ushauri Wa Baba Kwa Mwanae.
1. Mwanangu, mwanamke anaweza kuwa mkeo, mwingine anaweza kuwa mama
wa
watoto wako, lakini ukipata mwanamke ambae atakuwa kama mama kwako, mama kwa
wanao na mama kwa familia, tafadhali mwanangu usimuache huyo!
2. Usimfanye mwanamke wako kuwa ndio wa kupika na kufanya kazi zote za
jikoni peke yake, tabia hiyo sio nzuri Kwani hata nyakati zetu, mashamba yetu
yalijulikana kwa majina yetu wanaume lakini tulifanya kazi pamoja!
3. Kijana wangu, nikikwambia wewe ni kichwa cha familia, simaanishi
kutuna kwa pochi lako, usiangalie kabisa pochi yako, angalia kama utaona
tabasamu usoni kwa mke wako. Pesa sio kila kitu katika ndoa na haileti ukuu wa
familia!
4. Ukitaka kuwa na maisha marefu na ukapunguza misongo ya mawazo, ongea
na mkeo pangeni bajeti ya mahitaji yenu, kisha mwache mkeo awe na jukumu la
kuratibu mahitaji ya kila siku ya familia kwa kumkabidhi fungu husika hata kama
limetokana na michango yenu wawili. wanawake wanajua sana kupanga bajeti na hii
haitakuwa rahisi kwa yeye kutumia hela hovyo wakati akijua kuwa nyumbani kuna
mahitaji ya msingi, lakini hela zikiwa mikono mwako ataendelea kuomba hata kama
utakuwa umeishiwa!
5. Mwanangu, Usithubutu kumpiga mkeo, maumivu ya kipigo hukaa ndani ya
moyo wake kwa muda mrefu sana na huacha kidonda ambacho hukawia sana kupona. Ni
hatari sana kuishi na mwanamke mwenye majeraha moyoni!
6. Mwanangu, sasa unaamua kuoa,kama bado utaendelea kuishi maisha kama
ya ubachela na mke wako, sio muda mrefu utakuwa bachela tena. ukioa Badilika
anza kuishi maisha ya mke na mume!
7. Zamani,tulikuwa na wake wengi na watoto wengi kwa sababu tulikuwa na
mashamba makubwa na mavuno yalikuwa makubwa, lakini kwa sasa maisha
yamebadilika, kwa hiyo mkumbatie mwanamke wako peke yake kwani hakuna ardhi
tena na mahitaji ya watoto ni makubwa sana. Angalia ukubwa wa familia yako!
8. Mwanangu, chini ya mwembe ambao nilikuwa nikikutana na mama yako
inaweza kuwa ni hoteli kubwa kwa nyakati zenu,lakini kumbuka, kitu pekee
tulichoweza kufanya chini ya mwembe ilikuwa ni kukumbatiana pekee.nakushauri
ukikutana na marafiki wa kike kikubwa unachoweza kufanya nao ni kupeana mikono
na ikizidi ni kukumbatiana hadharani sio vinginevyo!
9. Mwanangu, usibadilike mara utakapoanza kupata mafanikio Zaidi,
kuliko kuwahudumia hao viruka njia wa mtaani ambao hawajui mmetoka wapi na
mkeo, nakushauri utumie na kufurahia mafanikio yako na mkeo ambae aliweza
kusimama imara wakati wote wa mapito yenu magumu.
10. Mwanangu, kumbuka unapoanza kusema au kuona mke wako kabadilika,
ujue kuwa kuna kitu ambacho ulikuwa ukikifanya umeacha kukifanya. Jitathmini na
anza kufanya au kutimiza wajibu wako.
11. Usijaribu kumfananisha au kumlinganisha mke wako na mwanamke
mwingine wa nje, kwani hata yeye anakuvumilia sana na hajakufafanisha na
mwanaume mwingine yoyote huko nje na ndio maana aliamua kuwa na wewe.
12. Sasa hivi kuna hiki kitu kinaitwa haki za wanawake, sawa,kama
mwanamke anasema ana haki sawa na wewe katika nyumba, basi gawanya mahitaji
yote ya ndani kwenu katika sehemu mbili zilizo sawa,halafu timiza nusu yako na
mwambie atimize nusu iliyobaki.
13. Mwanangu, nilimuoa mama yako akiwa bado kigoli (bikra) na nilikuwa
naenda sana kwao kabla sijamuoa, lakini kutomkuta mkeo bikra kusikufanye
umlaumu kuwa alikuwa muhuni, kumbuka wanawake wa enzi zetu na wasasa ni
tofauti, ulimchagua mwenyewe na ukigoli wake hukuujua kabisa. Usiingize mambo
ya kabla ya ndoa kwenye ndoa yenu.
14. Mwanangu, sikuwapeleka dada zako shule kwa kuwa nilikuwa mjinga
kama wazee wengi wa hapa kijiji wasemavyo, tafadhari usifanye ujinga huu, kwani
kiwango cha mafanikio ya wanawake sasa kimefanya wanaume waonekane ni watu wa kawaida
sana na sio muhimu kama enzi zetu. Ukijaliwa watoto wape elimu.
15. Mwanangu, zamani enzi za ujana wetu, wanawake walikuwa na urembo wa
asili, ingawa siwezi kukudanganya, wengine waliongeza urembo kwa kujichora hina
na hata kutoboa pua na masikio lakini usisahau hawakuonyesha maumbile yao nyeti
hadharani kama sasa. Hakikisha mkeo analijua hili!
16. Mwanangu, mama yako na mimi hatuna hisa katika kila kitu
kinachoendelea kwenye maisha yenu, jaribuni kutatua changamoto zenu wenyewe
bila kila mara kuja kwetu kuomba usuluhishi. Ndoa ni pamoja na ukomavu wa
kutatua changamoto zenu bila kuziuza kama gazeti kwa kila mtu.
17. Mwanangu,nilimnunulia mama yako kifaa cha kupikia vitumbua ili
aanzishe mradi wa kuuza vitumbua, pia nilimsaidia kununua cherehani yake ya
kwanza, tafadhari msaidie mke wako kutimiza ndoto zake kulingana na uwezo wako
kama ambavyo unahangaika kutimiza ndoto zako.
18. Mwanangu, usiache kutusaidia mimi na mama yako, utu uzima una
changamoto nyingi sana na Mungu akikujalia utaziona muda ukifika. Pamoja na
kutimiza majukumu yako kama baba wa familia kumbuka pia bado tunaishi na wewe
ni mtoto wetu.
19. Mwanangu, kila upatapo muda wa kusali, Sali na familia yako, kuna
kesho ambayo huijui, ongea na MUNGU wako ambae anajua kila kitu kila siku!
20.NAKUTAKIA MAISHA MEMA KATIKA
NDOA YAKO MWANANGU NAKUPENDA.
Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment