Sehemu Ya (131) : Yaani Ukiona Unajiandaa Saana Valentine's Day.. Kaa Ukijua Uhusiano Wako Una "Ufa".
Taratibu tutaelewana tu..
Unasubiria jumatano ya tarehe 14 kwa nguvu sana ILI
IWAJE? Labda kama ni
Anniversary ya penzi lenu (mlikutana siku ya tarehe hiyo) kwamba ni muhimu
kuadhimisha.. Wewe penzi lako na mchuchu mmeanza june 12 valentine inawahusu
nini?
Mwaka mzima ulikua wapi? Watu wenye mapenzi STRONG SIKU HII YA JUMATANO
NI YA KAWAIDA SANA na wataenda skylight tu thai village kama hamna
kinachoendelea , ila WEWE na uhusiano wako wa Bagia na Chumvi ndo unataka
ufufukie jumatano alafu jumapili mzike
tena mpaka mwakani. Kwangu mimi Valentine ni kila siku.. Nikikuta nguo nzuri ya
bebe nanunua nampelekea , hata kama ni november 19 Nikimmiss namfuata gheto
tunaenda Dinner cape town fish market kula.. akiona kiatu kizuri ana nunua
anani suprise , hata kama ni August 7..
Penzi lililokufa halitabustiwa na Valentine's day kamwe.. kama hupendwi
hupendwi tu , penzi halifufuki jumatano huo ni mkwara nje ya net.. penzi
lililojengwa kwenye misingi imara huenjoy Valentine kila siku narudia tena ,
ukiona umepania sana jumatano ujue penzi
lako lina shida kwasababu hata hata LEO inaweza kuwa Valentine yako
ukiamua. PENZI LA KWELI HALINA TAREHE KAMA KALENDA.
Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment