Sehemu Ya (130) : Ushauri Wa Kimaisha Kidogo Unaweza Jifunza Kitu Hapa.
Vijana wengi wamekua wakifikiria kuoa pindi tuu wanapoanza maisha ya
kujitegemea, kijana anapokua anamiliki geto, ana kitanda ka sofa ka TV ka jiko
ka gesi na tuvindoo twa kuhifazia maji hapo anajiona sasa anauwezo wa kuoa.
Kabla kijana hujaoa jitafakari kwanza unaplan maisha yako yaweje, uwe
mwenye pesa nyingi au uwe masikini mzuri, kama unahitaji kuishi maisha ya
kifahari basi tambua mwanamke anaweza kua kikwazo cha wewe kuendelea.
Pindi utakapo oa/ kuishi na mwanamke tambua utakua na familia tatu(3)
familia ya kwenu ,familia ya kwako na familia ya mke wako. Je upo tayari kubeba
mzigo mkubwa pindi ukiwa na umri wa utafutaji. Utashindwa kufanikisha malengo
kwasababu utakua na mzigo mkubwa.
Mwanamke anaamini njia bora ya yeye kutoka kimaisha ni kuolewa, hapo
ana rahisisha maisha yake yeye jamani mwanamke ni mzigo sana tena ni mzigo
mzito, usikubali kuoa ukiwa na umri chini ya miaka 26 wanawake wengi humfanya
mwanaune kitega uchumi chake.
Tafakari kidogo kipato chako ni sh ngapi kwa mwezi, utatakiwa uache
nyumbani sh.ngapi kwa siku(kodi ya meza). Ikitokea dharura utatakiwa utumie sh
ngapi hapo utagundua pesa yako itaishia kwenye matumizi ya kawaida, pesa ya
malengo itakua ni kidogo kuliko ya matumizi.
Utakapofikia kuoa basi fanya chaguo sahihi usichukue mwanamke eti
sababu ana makalio makubwa hayo makalio yake hayata kuongezea uchumi wako,
angalia mwanamke mwenye future, mwanamke anaefikiria utafutaji sio madada zetu
wanaofikiria kukufinyia kwa ndani.
NB; watu waliofanikiwa ki maisha baada ya kuoa ni wachache wakati mzuri
wa kujipanga kimaisha ni kabla ya kuoa.
Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment