Sehemu Ya (98) : Dada Zangu Ni Vizuri Kama Mkiyafahamu Yafuatayo.
👉 Mwili wako sio Maonesho, kila mwanaume auone.
👉 Mwili wako sio Mdoli kila mwanaume Auchezee.
👉 Mwili wako sio dampo, upokee kila uchafu wa mwanaume.
👉 Mwili wako sio Mali ya umma kila mwanaume akutumie.
👉 Mwili wako sio kiburudisho, kila mwanaume Ajiridhishe.
👉 Mwili wako sio pazia la Sebuleni, kila mwanaume Akufunue.
👉 Mwili wako sio "Diamond Karanga-Nogewa
Jirambe"
za kutembezwa mtaani kila
mwanaume Akuonje Utamu wako.
🔹 Mwili wako ni wa Thamani sana. Mwili wako ndio utu wako.
🔹 Ebu Tunza Mwili wako nao Ukutunze. Uheshimu Mwili wako nao
Utakuheshimisha.
🔹 Si kila mtu wa kuushika Mwili wako. Usitumie Mwili wako kama
kitega uchumi, Usitumie Mwili wako kama dhamana ya kupata vile unavyohitaji.
🔹 Usitumie Mwili wako kama Njia ya kupata Mume Atakayekuoa.
Kama Mungu amepanga Uolewe utaolewa tu dada yangu hata bila ya kufunua Sketi
yako. Muamini Mungu Yeye ndiye aliyeshikilia maisha yako.
🔹 Kuna mtu mmoja tu anayestahili kuugusa Mwili wako, kuuona
Mwili wako, kuujua Uzuri wako.. Msubiri, Usiwe na Haraka, Mungu atamleta kwako.
Endelea Kusubiri.
🔹 JITUNZE, JITHAMINI, JIKUBALI NA JIAMINI..!
Mwanaume Usiwe Kama Paka Kulamba Kila Sufuria Utalamba Sumu Ufe.
Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment