Sehemu Ya (96) : Binti... Nna Ushauri Kwa Ajili Yako Hapa.
Binti nisikilize mimi...
1. Mwanaume atakaekutambulisha kwa wazazi wake na si kwa rafiki zake
pekee huyo ndiye mwenye mwelekeo wa kufanya maisha na wewe.
2. Usitizame gari wala pesa nyingi ukadhani ndio kipimo cha utajiri wa
mwanaume, ndoto na maono yake yenye tija ndio muelekeo mzuri wa utajiri wa
mwanaume.
3. Binti yangu, ni wazi kwamba mwanaume anaweza akakupa talaka au
kukufukuza kwake, ila elimu, ujuzi na kipaji hakiwezi kukupa talaka. Hivyo basi
focus katika kupata elimu na ujuzi kabla hujampata mwanaume wako.
4. Binti yangu mpendwa, usikubali ngono ikufanye kuwa mama kabla ya
ndoa kukufanya kuwa mke. Tangulia kwanza kuwa mke ndipo uwe mama.
5. Wanaume bora sio vigumu kuwapata, ila ni vigumu kuwavutia. Hivyo
basi kama unataka mwanaume bora jiandae kumvutia. Si kumvutia kimapenzi! La
hasha binti yangu..namaanisha kuwa na tabia na siha njema anayokufunza mama
yako.
6. Matokeo ya kuwadharau wanaume walio bora na kujichanganya na wanaume
matapeli ni kwamba utakuja kuchanganyikiwa, hasira na visasi pale utakapoona
wale wanaume bora uliowadharau wanaoa wanawake ambao nao uliwaona kama sio
wazuri kama wewe.
7. Binti yangu, kama utamuuliza Mungu ni nini kanuni ya uchumba ni
rahisi tu; Kama huyo Mwanaume hana Mungu, basi hastahili kuwa na wewe.
8. Bibi yako enzi za ujana wake alikuwa mzuri kweli, sasa nakupa agizo
hili, kila utembeapo tembea na picha ya bibi yako katika pochi yako. Ili kila
utakapoifungua pochi picha itakukumbusha kwamba uzuri ni wa muda tu, ila tabia,
hekima na busara zinadumu milele.
9. Jipende na ujitunze, wewe ni hekalu la mwenyezi Mungu, Mungu
hatapenda kuona hekalu lake likichafuliwa.
10. Hakuna mpumbavu mkubwa kama mwanamke ambae anamdharau mwanaume kwa
sababu ya hali yake ya kiuchumi aliyonayo kwa wakati huo.
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment