Sehemu Ya (95) : Mambo Ambayo Hupaswi Kumfanyia Mwanamke Anayekupenda Kwa Dhati.
2. Usi 'pretend' unampenda ili ufanikiwe kufanya yako.
3. Mtukane vyovyote vile ila sio wazazi wake na kumwambia kuwa yeye ni
mbaya.
4. Usimfananishe na wanawake zako waliopita.
5. Usimchukulie kirahisirahisi (Never take her love for granted)
6. Usimpige.
7. Usimsaliti na kuonyesha kabisa dharau ajue kuwa una 'cheat'
8. Usimvunjie heshima kwa kumgombeza mbele za watu.
9. Usimpotezee muda wake kama hauna mpango wa kumuoa, unamchelewesha
kupata mume bora.
10. Usimfanye ajione hapendwi na ana mkosi hapa ulimwenguni, huo ni
ujuha.
11. Usimbake
12. Kamwe usisahau kumwambia unampenda na yeye ni mzuri hiyo haipunguzi
nguvu za kiume.
13. Usimpe mimba na kumkimbia au kumwambia aitoe, kama huna nia ya
kumuoa achana na hayo mambo, nadhani unajua kabisa matokeo ya kufanya ngono.
Sometimes sisi wanaume ni pasua kichwa vilevile, unakuta tunapata
mwanamke anaekupenda kwa dhati, mwanamke ambae ni potential, mwanamke ambae
hakodoi macho pochi yako, ila masikini ya Mungu anaishia kuumizwa na kulia kila
siku na kujilaumu kwanini alikupenda.
Wewe fanya hivyo ukidhani unamkomoa, ila siku na wewe ukibananishwa na
mwanamke mjasiriamwili utaisoma namba, nakwambia utauza hadi boxer.
Baadae unakuja kulalamika hapa 'wanawake wanapenda pesa, wanawake
wanapenda pesa.' ukishikwa shikamana. Na kama humpendi usimtongoze.
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment