Sehemu Ya (92) : Ladies, Msiwakatie Tamaa, Wanaume Wenye Tabia Zifuatazo..
WANAWAKE NISIKILIZENI MWALIMU WENU... MI SIO MWALIMU KIPOFU.
1. Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje.
Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli.
2. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa,
hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende
mwanaume huyu.
3. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake. Anaongea nao vizuri na
kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume!
4. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi
kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka.. sio wa
kumuacha huyu!
5. Hakulazimishi kufanya mapenzi. Anakupenda sana kiasi kwamba hawezi
kukulazimisha jambo ambalo hauko na hiari nalo. Yupo karibu na wewe wakati wote
na sio tu anapokutaka kimapenzi, huyu ni bonge la bwana.
6. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la
kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana mkono
wa birika, Huyu anakupenda!
7. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe,
huyu anayo dhamira ya dhati kutoka moyoni mwake ya kukufanya uwe mkewe.
Hizi ni moja ya dalili kwamba mwanaume wako anakupenda na anataka
atengeneze future pamoja na wewe. Usikate tamaa juu ya mwanaume wa aina hii.
Hao wenye sixpack sijui eight pack, wabeba vyuma, wavaa milegezo,
wanyonya midomo na mahandsome wavaa hereni, waume za watu, masupa staa, watoto
wa vigogo, hawatakusaidia lolote, utabaki ukiumizwa tu moyo wako.
Kabla hujajipendekeza kwa wanaume wa aina hiyo, jiulize wanawake
wanzako wangapi wameshajipendekeza kwa sababu ya hizo pesa zake, hivyo na wewe
unajiongeza kwenye foleni!
Mvumilie mwanaume wako, anazo ndoto njema, mapenzi ya kweli ni vigumu
sana kuyapata. Ila pesa na mali ni rahisi sana kuzipata kama utajibidiisha.
Usipende mitelemko, mitelemko mingine ni njia ziletazo mauti! -
Ukishikwa shikamana, ukipendwa, pendeka!
My wisdom, "Don't date a rich man, date a GOOD MAN, Good man will
spend his life trying to keep u happy, no rich man can buy that!"
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment