Sehemu Ya (93) : Wanaume Mambo 10 Ya Kuzingatia Saana Katika Mahusiano Na Maisha Pia.
UJUMBE MUHIMU KWA WANAUME WOTE.
Katika maisha mwanaume inakupasa kufahamu mambo ya msingi yatakayo
fanya maisha yako yawe ya furaha, mambo hayo ni pamoja na:
1. Oa mwanamke ambae unaweza KUSALI nae na sio kwa sababu anajua
KUFANYA MAPENZI vema.
2. Mwanaume bora KAMWE hapimwi kwa idadi ya wanawake alionao au
aliotembea nao BALI kwa idadi ya wanawake aliowaambia "Mimi ni mume wa
mtu" au ninae mtu tayari.
3. Kuna aina ya wanawake unatakiwa kuwaepuka kabisa kwa gharama yoyote
ile, "wanawake wamaodhani uzuri wao ndio bora zaidi kuliko tabia zao"
4. Kila mwanamke anavutia akivaa nguo fupi inayoonesha maungo yake
wazi, ila kama utakuta mwanamke amevaa nguo ndefu au za kusitiri mwili wake na
bado anavutia, huyu ni dhahabu! Anathamini mali za mumewe!
5. Kamwe usimpe mwanamke mimba ya mtoto kabla hujampa mimba ya malengo
na ukayatimiza.
6. Tafuta mwanamke ambae atakupa changamoto za maisha na kuongeza uwezo
wako wa kufikiri na sio mwanamke wa kila kitu Ndio mzee!
7. Wanawake wakamilifu hawapatikani popote duniani, ila wanawake bora
wapo kila mahali.
8. Mwanamke anaweza kukusaliti, ila Mungu hawezi kukusaliti, hivyo basi
kabla hujapata mwanamke Mpate Mungu kwanza. Kuna raha sana kuwa ndani ya Mungu
asikwambie mtu!
9. Kama unajijua umefikisha miaka 25 na kuendelea epuka mambo ya
kivulana, kuvaa suruali katikati ya makalio, kuvaa hereni, kubadili badili
wanawake kama unachambua mitumba ya karume etc.
10. Usitumie kichwa chako kunyoa kiduku, tumia kichwa chako kuwaza
mambo yenye tija ikiwemo kutafuta pesa na kuongeza hazina ya maarifa.
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment