Sehemu Ya (86) : Wanaume Mnawajua Wanawake Penzi-Umeme??


Ukitaka Usimegewe hakikisha unampa Mpenzi wako Mahaba-Niue Niteketeze
Kabisa yenye Megawati za kumtosha kuendesha Mitambo ya Furaha kwenye Moyo wake...

Ukishindwa kumpatia lazima atakutafutia Jenereta la dharura au Solar Panel just incase Umeme-Penzi wako hautabiriki.

Hakuna Mtu anayependa kukaa gizani kusubiria Umeme usiotabirika wa TANESCO wakati Majenereta yanauzwa. Ukitafutiwa Jenereta la Dharura kwenye Mapenzi usilalamike, Jilaumu mwenyewe kwa kutotabirika kwa Umeme-Penzi wako... Watu wanasikia Joto wameamua kujizatiti ili ukikatika tu kitu kinawaka AUTOMATIC.

Shikamoo wote mliowekeza mitambo ya Symbion na Aggreko kwa sababu Wapenzi wenu wapo-wapo tu hawajitambui wanatumia Mita au Unit za LUKU.

WANAUME:Msipoangalia mtajikuta LUKU haina kazi mtu yuko under Generator masaa 24 kuepuka kadhia, Utajibebaje!... chura anapenda kuoga Maji lakini sio na sabuni.

Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies 
WhatsApp +255 715 758 021

No comments