Sehemu Ya (82) : Madhara Ya Kutopenda Unapopendwa.. Jifunze Kitu Hapa.
Demu wako anakutumia Meseji kwa upendo kabisa wala hutikisiki kumjibu,
au
umemjibu meseji 2 ili kumridhisha aache usumbufu ukamwambia uko Bize..
anatamani aendelee kuchat na wewe mara kwa mara coz anakupenda lakini
umemuwekea Barriers.. Umeweka Ukuta...
Unaona Ujanja madai yako... Unamwambia
Mpenzi wako uko bize ili aache kukusumbua kumbe wewe uko Bize unachat na Wanawake
wengine Freely... SUBIRI UTAONA.
Akitaka kukuona Mspend Weekend pamoja ili kuendelea kujenga ukaribu
unamjia na visingizio, Mara Mama kaniita Home... Mara Baba kanituma kwa
shangazi Mbagala.. Mara sijisikii vizuri ntalala tu nimechoka leo.. Mara Sina hela
sitoki..
Ilimradi umkwepe usiwe nae, kumbe hujatumwa kwa Shangazi wala mama
hajakuita, unajiiba unapeleka zawadi za Maua kwa mdada mwingine huku umemuacha
Mpenzi wako kajikunyata Home kaboreka. Hujui tu Mpenzi wako amekataa Mialiko
mingapi ya Vibolo-Dinda ili awe na wewe, Mwanaume anayempenda!
WE MWANAUME ACHA UJINGA! Unahangaika kuweka Bati Nyumba ya Jirani
wakati Nyumba yako umeezekea Makuti na Inavuja, Hiyo akili au matope?? Charity
Begins At Home... Pendeni mnakopendwa vijana.
We jifanye mjanja sasa, ipo siku
atachoka halafu siku moja utakuta Masela wajanja wamemgeuza demu wako Tiger
Woods wanashindana kutumbukiza Mpira wa Golf tunduni.. SUBIRI UTAONA!
Kwa Hisani ya wanaume wote mliozama Dimbwini! Wadada wenye vyeti vya
form four mpo ???? tafuta cheti uolewe naona albadiri inafanya kazi.
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment