Sehemu Ya (81) : Sio Kila EX Wako Anayeomba Mrudiane Anamaanisha.


Sio Kila EX wako anayeomba Mrudiane anamaanisha! Wengine huomba kurudi ili
wakutesti tu jinsi ulivyo Mbulula, jinsi usivyo na msimamo na jinsi ulivyo CHEAP na huna Misimamo wala Future.

Jitu mmeachana miezi 6, leo linakutesti lirudishe majeshi, na wewe ulivyo kiazi, upo-upo tu, ina maana miezi yote hii ulikuwa umeganda unasubiria rehema zake ama??

Kurudia Matapishi ya EX ukitegemea Amebadilika ni Sawa na Kupika Sufuria la Makande kwa Mshumaa, Utaambulia Masizi tu.. Kipi kipya kakiona kwako hadi arudi?? Nini Kilimshinda huko nyuma ambacho leo anakiweza anataka kurudi?? Akafie Mbele huko.


KUWA NA MSIMAMO, Ukisema Its Over umaanishe, sio unakuwa na hisia zinapepea tu kama Bendera ya Katibu Kata wa Kigogo Luhanga... Mtu kama Hajielewi achana nae, siku akijirudisha mwambie kwanza akapimwe mkojo kwa mkemia Mkuu.

Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies 
WhatsApp +255 715 758 021

No comments