Sehemu Ya (78) : Jinsi Wanawake Sikuhizi Wanavoigiza "U-Wife Material" Katika Kusaka "PETE".
wameshibana.. wanapendana... yaani ukiwatazama unaona YEESS, Natakaa kuwa kama
wale..
Walipooana ukacheza kweli ukumbini, lakini ghafla baada ya mwaka
unaanza kusikia kwamba Yaliyomo Hayamo.. Ndoa hakukaliki... Mdada kabla ya Ndoa
alikuwa anajifanya kupeleka Vitenge kwa 'wakwe', akifika anasalimia kwa magoti
hadi chini anaburuza goti getini hadi dining, wazazi wakasema Yes.. Mwanaume
nae akaona Haleluyah wife material si ndo huyu....
Mwanamke kaomba reserve key,
unarudi home unakuta nyumba imepangwa, imedekiwa na Dettol, inanukia Lady Diana
Air Freshener, Tiles za bafuni zimesuguliwa na kung'arishwa na Sabuni Maarufu
kutoka BUBBLY STORES Mikocheni.. Ukitoka job unavuliwa Boxer zinalowekwa,
unapewa Massage hadi unasinzia, unalishwa dinner kitandani...
Mwenyewe
ukatangaza Ndoa... Umefika Ndani Mwanamke kabadilika, hapigi goti, kiburi
mtindo mmoja, Usafi sifuri, ye mwenyewe kuoga hadi asikie wageni lasivyo
anashinda na kanga nyonyo wazi.. Kiburi kwa Wakwe waliompigia kura ya Veto
aolewe kwa kuwa na adabu.. Ndugu wa mume...
Kwa kifupi Umeoa Mtu MWEKUNDU halafu baada ya Mwaka anakuwa wa
BLUU-BAHARI, anaekti U-Wife Material kusaka PETE, akishaipata sasa ndo unaona
Rangi Halisi Usiwe Kinyonga Bishosti, kama ni mchafu Muonyeshe akupende na
Kikwapa chako.. Kama una kiburi Onesha ajue anaoa Bumunda...
Sio unajifanya
mtaalamu wa kufua Boxer halafu ukiolewa unasema, 'Baby siwezi kufua Jeans zako
Kucha zangu zinakatika', zikatike zimekuwa StejiShoo wa Baikoko??? SHOW UR TRUE
COLOURS.
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment