Sehemu Ya (71) : Ushauri Kidogo Kwa Wale Walioko Kwenye Dimbwi La Mapenzi Na Wanapitia Mapito.
wengine na kuwa na wewe. Ulimwambia unampenda kweli na utamjali kwa shida na raha
ndiyo maana alikuamini na kukukabidhi funguo ya mwili wake
Ulimwambia kamwe huwezi kumsaliti, hakukuamini katika hilo
lakini ulimthibitishia tena kwa unyenyekevu na upole akakuamini na kukuomba
usije kumuumiza.
Ulimuahidi na kumwambia wewe si kama wale wengine
hutamuumiza moyo, hutamtesa moyo wake ukasema wewe ni wa tofauti na wale
waliomuumiza.
Umesahau yote uliyoahidi, umesahau yote uliyosema
hutamfanyia, leo hii unatesa, leo hii unamtoa machozi hujali tena hisia zake,
leo hii umekuwa chanzo cha yeye kukosa furaha na amani, leo hii hutaki hata
kusikia tena, leo hii unaona hana maana, leo hii unamuona takataka na kuona
hana sifa za kuwa na wewe.
Leo hii mtoto wa watu ushampotezea dira ya maisha yake,
harafu unamkataa na kuona si kitu, unajua ni kiasi gani anaumia? Unajua ni
kiasi gani anapata mateso kwa akili yako?
Mungu hawezi kukuacha pekee yako, wewe upitiaye shida hizi,
Mungu hawezi kuona unapata shida hizi akakuacha, tambua kuwa chozi lako
haliendi bure, na elewa kuwa malipo ya kila kitu ni hapa hapa, jipe moyo kwani
kesho utasimama tena, Mungu amemwandaa mtu wa kukufuta machozi yako, Mungu
amemuandaa mtu wa kurejesha furaha yako. Nmeshindwa kuwashauri wote poleni sana.
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment