Sehemu Ya (70) : Story Fupi Ya Wanandoa.. Unaeza Jifunza Kitu Hapa.
Aliamka akiwa na uchu wa tendo la ndoa. Akaanza kumpapasa
mkewe. Taratibu akainuka upande wake na kulala juu ya mkewe huku akianza
kumbusu. Lakini mkewe hakuwa na ushirikiano kuonesha kuwa hakuwa tayari.Mume akaendelea, akambusu shingoni, na kuanza kumtanua
miguu..lakini mkewe akabana miguu zaidi. Mume akakasirika...
"Nini tatizo?" Mume akauliza.
"Sisi tuna matatizo" Mke akajibu.
"Unamaanisha nini? Mimi sikuelewi" Mume akauliza.
"Kitu pekee tunachoshirikiana vizuri pamoja ni tendo la
ndoa tu" Mke akajibu.
"Nilifikiri unafurahia tendo la ndoa na mimi. Tizama
nimekua muaminifu kwako. Sijawahi kukusaliti na wewe ni shahidi wa hilo. Sasa
nini tatizo mpaka unanizuia?" Mume akamuuliza mkewe.
"Ni kweli. Unanifanya vizuri. Nafurahia. Lakini ndoa ni
zaidi ya sex. Haitoshi kuwa muaminifu pekee, ndoa inahitaji kuwa na kina,
maongezi, mipango na mashauriano sio sex peke yake basi..."
...Sipendi tuwe nafsi mbili ambazo zipo tupu. Nakumbuka
mwanzoni mwa ndoa yetu, tulikua vizuri. Nahitaji tuongee, tucheke, tusali
pamoja, twende out kama zamani, tukumbatiane, tutengeneze kumbukumbu, tucheze
na watoto wetu na tutembee maeneo mbalimbali ili tuwe na intimacy katika ndoa
yetu...
...Kitu ambacho tunacho sasa hivi sio ndoa, bali ni mipango
ya sex tu. Sex is just not enough" Mke akaongea kwa kulalamika.
"Ooh! Huu ni ukweli" Mume akajibu.
"Ukweli mchungu haswa" Mke akapigilia msumari.
Mume akaanza kupapasa nywele za mkewe taratibu na kuanza
kuongea....
"Umeongea ukweli. Mambo yamebadilika sana tokea tupate
watoto. Nafikiri ubize nao umechangia vivyo hivyo maisha yamekuwa tight
sana."
Mke akamtaza mumewe na kuongea,...
"Darling watu hutengeneza muda kwa lile jambo lililo la
muhimu. Kila jambo linalo wakati wake. Nahitaji niwe zaidi ya mama wa watoto
wako tu, mimi ni mke wako. Nahitaji nijisikie kama mke wako na mwanamke wako
unaenimiliki...
...Nahitaji muda wako mzuri kama uliokua ukinipa zamani. Sio
mwingi. Kidogo tu. Nahitaji kupendwa nahitaji tuwe na maongezi. Nahitaji muda
wetu wawili mimi ma wewe tu. Ni lini mara ya mwisho ulinipapasa nywele zangu
kama unavyofanya sasa hivi?"
"Ni muda mrefu sana, hata sikumbuki ni lini". Mume
akajibu.
Mke akaweka kidole chake kwenye lips za mumewe na akaendelea
kuzungumza....
"Exactly, hujawahi kuchukua muda wako kunitizama kwa
sababu kila siku upo busy tu. Unajua mwanamke haombi mambo mengi sana. Hata
kitu kidogo tu kama hiki cha kunipapasa nywele zangu kinanigusa moyo wangu na
kuona ni namna gani unavyonithamini...
Mke akaendelea....
...Wanawake wengi wamechoka na tendo la ndoa katika ndoa
zao. Wana-fake orgasms, wanasingizia vichwa vinauma, wanasingizia kuchoka au
hata kudanganya kuwa wako kwenye period ilimradi tu kukwepa kufanya mapenzi na
waume zao kwa sababu hawajioni kama wanapendwa tena.
...Mimi nataka kupendwa mume wangu, sitaki kuwa kama hao
wanawake. Hii nyumba yetu sio Lodge ya wewe kuja kulala, kufanya mapenzi na
mimi na kuondoka. Hii ni nyumba yetu, kitanda chetu cha ndoa na tunayo ndoa
halali kabisa..nakuhitaji mume wangu.."
"Nakuhitaji pia mke wangu, maneno yako yameniingia
vilivyo. Ni kweli, muda pekee ninaokugusa ni wakati wa tendo la ndoa tu.
Nimekua busy mno kiasi hata nimeshindwa kutafuta muda mzuri wa kuwa karibu ma
wewe. Nakuahidi kuanzia sasa nitabadilika...
...Umenifundisha kitu cha muhimu sana, kwamba, watu
hutengeneza muda kwa lile jambo lililo la muhimu. Wewe ni wa muhimu kwangu.
Nitatengeneza muda wako. Muda wa watoto na muda wa kazi..." Mume akaongea
huku akimsogelea mkewe na kumbusu. Busu lilikuwa tamu, sio la haraka na sio la taratibu. It was
intimate.
Mume akaweka kichwa chake kwenye kifua cha mkewe chenye joto
kilichobeba maziwa mithili ya embe dodo mbivu. Na kwa muda kidogo wakaanza
kuongea na kutaniana huku mke akichezea vidole vya mumewe.
Wakacheka pamoja, wakazungumza mambo mengi na hisia zao
zikaunganishwa pamoja. Na bila kujielewa wakajikuta wakishiriki lile tendo
takatifu lililo halalishwa kwao. Mke akampa mumewe haki yake kwa uhuru wote. Na
mumewe akafurahia na kuburudika.
Kuanzia hapo, ndoa yao ikajengwa kwa msingi wa maelewano na
wala sio sex peke yake. Na pale walipofanya sex haikuwa sex pekee bali ilikuwa
ni Love making.
Have you made your marriage empty as you hide behind sex? There
is more to marriage than sex.
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment