Sehemu Ya (62) : Je, Unayajua Mapenzi Ya "SERIES"?

Upendo wa kweli hupimwa pale Mambo uliyomuona nayo Season 1
yanapobadilika ikifika season 2, Upendo wa kweli hupimwa pale ambapo Hela ulizomkuta nazo wakati mnaanza zinapokwisha na inabidi msaidiane kutafuta zingine ili muendelee kuishi vizuri kama Mwanzo Upendo wa kweli hupimwa pale Umbo lake linapofifia na ile Mijihips uliyompendea mwanzo inapokwisha.

Ukimuacha kwa sababu lile tako refu ulilomkuta nalo akiwa Kigoli mbichi limekwisha HUKUMPENDA YEYE, ULIPENDA TAKO ZAIDI. Ukimuacha kwa sababu yale maisha mazuri aliyokuwa anakupa mwanzo hayapo tena kwa sababu Uchumi umeyumba HUKUMPENDA YEYE, ULIPENDA MAISHA MAZURI ULIYOMKUTA NAYO.

Huwezi kuihama CHADEMA kwa sababu tu Halmashauri Kuu imemvua Uanachama Zitto Kabwe, Hukuipenda Chadema ila ulimpenda Zitto Kabwe. Jiulize leo, Unampenda yeye au Unapenda ulivyomkuta navyo?? Wengi wanafeli hapa, wamekuta Goodlife na Bata Love ikajiconnect fasta, Hela ikikata ndo utajua unatumia Wireless ya 4G LTE au uliweka Bundle ya Siku... 

Kuoa au kuolewa ni majariwa Tuombe Mungu kuna watu kipindi cha boyfriend mna machaguo mengi mnataka six packs wengine mnataka chura mnaishia kuoa mijusi .


Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies 
WhatsApp +255 715 758 021

No comments