Sehemu Ya (61) : Ladies, Mnawajua Wanaume Zipu Single Batani??

Mswaki ni kifaa ambacho kinatakiwa kutumika kwa ajili ya kusafisha Kinywa cha 
mtu mmoja tu... Sijawahi kuona mtu anashea Mswaki na babake kisa anampenda, au anamwambia 'Shangazi tumia tu haina shida'

Naongelea wale Wakaka ambao Zipu zao ni aina ya Singo Batani, zinafunga kifungo cha juu huku kitambi chote wazi... Zipu zao hazifungi kuficha Miswaki yao, wanashare Miswaki yao na watu wa4 tofauti, wa5 na kadhalika, Midomo mingine ina fizi zina damu, vinywa vingine vina harufu kama Dustbin ya Mamantilie.. 

Heshimuni Miswaki yenu kwa sababu inapaswa kusafisha Kinywa kimoja tu sasa we unaosha kila mdomo maana yake hujipendi mdomo wako ipo siku utaumwa maana magonjwa ya vinywa vyote ulivyosafisha utahamishia kinywani kwako!


Tulizeni hiyo miswaki yenu jamani maana mmeigeuza kama Mifagio ya Budege mnafagia-fagia tu kila uchafu.... Na wewe mdada unajua kabisa huo Mswaki una mtu umetumika na wewe unakinga domo lako, si utafute wa kwako? 

Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies 
WhatsApp +255 715 758 021

No comments