Sehemu Ya (60) : Jinsi Huruma Inavyowaponza Ladies Kwenye Mahusiano.. Siku Zoote.


Una Boyfriend, Unampenda ile mbaya, anajua unampenda na hufurukuti,
anakusumbua kwelikweli, wewe na kisima cha machozi ni Mutual Friends, kwa mwaka unalia mara nyingi kuliko Kikundi cha Waombolezaji wa Kinyakyusa... Imefikia muda unahisi Moyo wako umepigwa Ganzi, ukasema Enough is Enough... 

Ukaamua kumpa Moyo Mwanaume fulani, akaupokea ule moyo kama umetengenezwa na kioo, kwa heshima zote, na anautendea haki... Yule Kinabo aliyekutesa kwa miaka mingi ndio anashtuka, anajirudisha rudisha na kujiweka weka karibu kutafuta Bluetooth Network kwako, wakati wewe umepata Love of your Life.... Usivyo na akili, kisa amekuja kwako analia unahisi fisi kageuka beberu, eti unamwonea huruma... 

Mwanaume kulia machozi feki ni rahisi kuliko Mbuzi kutembea huku anamwaga kinyesi cha Karanga... Huruma yako itakuponza, utampoteza Mpenzi wa Ukweli na kurudi kwa janaume feki na mwisho unakosa vyote... Huruma mwisho Chumbe! .. Eeh Mungu wasamehe hawajui watendalo hata Maji yana aina Maji magumu na laini ... na vivyo hivyo na kwa viumbe wako.

Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies 
WhatsApp +255 715 758 021

1 comment: