Sehemu Ya (119) : Ladies, Hujaolewa Na Bado Unampa Jamaa "One Night Stands Na Blow Jobs" Zingatia Haya.

Kama wewe ni mwanamke na haujaolewa na upo kwenye mauhusiano na
mwanaume ambaye haujafunga naye ndoa  basi zingatia hili, linaweza kukusaidia na kukupa nuru nzuri ya ndoa bora yenye tija katika maisha yako ya mauhisiano.

Chagua mwanaume bora kwa kutizama utashi wake na mawazo yake chanya, mwanaume bora ni yule aliyekuzidi utashi, tabia nzuri pamoja hekima na busara na mwenye mapenzi ya dhati kwako.

Mwanaume anayekufaa ni yule  anayekujali  na kukuheshimu , mwanaume bora ni yule anayekupa mawazo ya kesho akiwa leo, mwanaume anayekufaa ni yule anayekufuta machozi na asiyekuliza kila siku .

Dada yangu tafuta mwanaume ambaye ni kichwa ili wewe uwe shingo sababu hakuna kichwa pasipo shingo.

Tengeneza mwanaume wako bora, anza naye kwenye maisha ya chini mkipeana faraja na matumaini ya kutengeneza ndoa bora na yenye mafanikio ya kipesa, na mauhisiano yenye afya yaliyo na mapenzi matamu na bora, usipende wanaume wa wanawake wenzio mtengeneze handsome wako.

Dada yangu achana na mabrothermen wanaopaka poda ,wanawanaotembea na selfiestick  hawana tija, mwanaume bora havai mlegezo (sag trousers) wala suruali za kuchanwa chanwa.

Mwanaume bora hata kama hana pesa daima huwa na hazina ya mawazo na ndoto zenye matumaini ya kuwa na future nzuri baadaye. Achana na wanaume maarufu  wengi wao hawana mapenzi ya dhati wanapenda kuwatumia wanawake kwa tamaa zao za mwili.

Dada yangu mimi nakupenda na natamani uwe na ndoa bora na uchague mpenzi bora, mpende mpenzi wako kwa moyo wote achana na zile kauli za wanaume wote wanafana.

Muombe Mungu akupe mume bora na wewe uwe mke bora sababu mke mwenye mapenzi ya dhati huwa anabeba baraka za mafanikio ya mume wake. Tafakari mauhusiano yako yapoje.

Wakati ni sasa sio kesho acha kuwa na idadi kubwa ya wanaume, chagua mwanaume wako mmoja bora, pia achana na utamaduni wa kuchat na ma ex.wako .

Tengeneza mume wako bora achana na wanaume wadhaifu na wasio na tija kwako chagua wanaume bora kwa sifa za ndani na sio kwa ubora wa nje.

"If a girl ever steals your man, there's no better revenge than letting her keep him. Real men…can't be stolen."

Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Ili Kupata Posts Zangu Kirahisi Zaidi Kwenye Simu Yako.http://www62.zippyshare.com/d/FvrvpQQg/31722/xxlbongotz.apk
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies 
WhatsApp +255 715 758 021

No comments