Sehemu Ya (118) : Mwaka Mpya Wa Mapenzi Yako, Badili Mtizamo Wako Hapa.

Ni ukweli usiopingika upo kwenye mahusiano yenye kero na maudhi ya hali ya
juu, yamkini unawaza namna ya kujikwamua kwenye mahusiano hayo lakini inashindikana kwakuwa umepoteza vitu vingi vya muhimu kwenye mahusiano hayo.

Mwaka Jana uwenda ulikuwa mwaka wa maumivu makali, machungu na changamoto kibao katika mahusiano yako, mwaka huu usikubali kufanywa zezeta tena,  BADILI MTAZAMO WAKO.

Umevumilia mateso, manyanyaso, dharau na kejeli yote hiyo ni kumdhihirishia ni kiasi gani unampenda lakini ikawa tofauti na mtazamo wako, mwaka huu usikubali BADILI MTAZAMO WAKO.

Umepoteza muda wako, gharama zako, umemtamburisha kwa watu wako muhimu lengo ni kumfanya awe wako wa milele ila bado anaku_cheat, usivumile atakuletea maradhi huyo, BADILI MTAZAMO WAKO.

Umemsomesha na kumtafutia kazi, umempa kila anachohitaji, mmevalisha pete za uchumba lakini sasa amekuona huna thamani, huna lolote na hata kukuzalilisha kwa marafiki zake  kutokana na udhaifu wako wa kibinaadamu, mwaka huu usikubali kuumiza akili yako juu yake, BADILI MTAZAMO WAKO.   
   
Amekupa mimba kirahisi rahisi tu kwa kigezo cha kukuoa ila hadi umezaa  bado hujajulikana kwao wala hajulikani kwenu na wewe bado unasubiri hiyo ndoa, shtuka sasa mtu wangu kabla  hajakuongeza mtoto wa pili wa nje ya ndoa hebu BADILI MTAZAMO WAKO.

Acha kuendelea kuvumilia pasipo na matumaini, kila kitu kinapangwa na MUNGU, uwenda huyo ulienaye si mpango wa MUNGU, BADILI MTAZAMO WAKO SASA, Usiendelee kuvumilia hisia zako kuchezewa na mtu asiyejua thamani yako, acha kuwa mtumwa wa ngono, Badirika sasa.


Nawatakia kheri ya Mwaka mpya Wa Mapenzi Yako,  bila shaka huu ndio mwaka wa mafanikio yako usikubali kupotezewa muda kirahisi rahisi kwa kubembeleza mapenzi yasiyo na tija,  usikubali kuwa zezeta. BADILI MTAZAMO WAKO.

Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Ili Kupata Posts Zangu Kirahisi Zaidi Kwenye Simu Yako.http://www62.zippyshare.com/d/FvrvpQQg/31722/xxlbongotz.apk
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies 
WhatsApp +255 715 758 021

No comments

a