Sehemu Ya (109) : Mwanaume, Ukifanywa Bwege Kisa Umependa Unapaswa Kucharazwa Viboko Mpaka Huo Ubwege Ukutoke.

My brother, nguvu yako kama mwanaume haionyeshwi kwenye stamina yako
katika tendo la ndoa peke yake. Eti kwa sababu unamfikisha kileleni mara tano, ambapo kimsingi ka-fake orgasm, haimaanishi kwamba wewe ndio kidume cha mbegu.

Hakuna haja ya kumbiringisha sarakasi zote katika sex kitandani na kumfanya anene kwa lugha zisizofahamika chimbuko lake, ili umuonyeshe kwamba wewe ni kidume haswa.

Mwanaume yeyote anaekula lishe sahihi, au wafanyao kazi ngumu kama kupasua mbao na kubeba zege nao wanaweza kufanya hivyo. Kama unataka kumuonyesha wewe ni mwanaume haswa, mthamini, mjali, provide for her na umpe attention kwa asilimia 120!

Kuwa mfalme wake na mfunike kwa upendo uliojawa uaminifu. Msikilize na ujivunie kuwa nae. Tambua potentiality yake aliyonao. Mlinde na umpende sana ili hata aweze kujiamini mbele za rafiki zake na kuwaambia kwamba "i'm in Love".

Wanawake wengi wanahofia hata kuwatambulisha wanaume zao kwa sababu hawana uhakika na kesho yao. Achana na kasumba iliyojengeka miongoni mwa jamii zetu eti kwamba ukimpenda sana mwanamke anakufanya bwege. Kwani wewe umeshikiliwa akili zako mpaka mwanamke akufanye bwege?

Unafikiri kwa nini tunaagizwa kuwapenda wake zetu na wakati huo huo tunahimizwa kuishi nao kwa akili. Mwanaume ukifanywa bwege kisa umependa unapaswa kucharazwa viboko mpaka huo ubwege ukutoke.

Wewe mpende na umuonyeshe hilo, kuwa nae karibu anapolia hata anapocheka... tengeneza kumbukumbu bora pamoja nae.. wanawake wanakumbukumbu ya haraka kwa sababu wanapenda kukumbuka yale mazuri uliyoyafanya.

Nguvu zako kama mwanaume hazipo katika sex pekee. In fact wanawake hawapendi sana sex... na anaweza akaipata popote pale, anachohitaji ni wewe tu na hapo hata hiyo sex ataifurahia!  Can you be her man?


Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Ili Kupata Posts Zangu Kirahisi Zaidi Kwenye Simu Yako.

Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies 
WhatsApp +255 715 758 021

No comments