Sehemu Ya (101) : Tawasikia Etii.. "Mi Siwezi Kushindana Na Mabinti Wadogo Wa Mjini."
Alikuwa akisoma article fulani kwenye mtandao huku amekaa kwenye kiti
kilichopo chumbani mwao..
"Darling...." Akamuita mumewe..
"Yes.." Mume akaitika...
"Unanipenda?" Akamuuliza mumewe ambaye alikuwa busy akifunga
tai tayari kwa kuivaa shingoni.
"Of course nakupenda my love. Nakupenda sana tu." Mume
akamjibu.
Mke akamtazama na kumwambia.."Kuna makala naisoma hapa inasema
kwamba asilimia 52 ya wanaume wanasaliti ndoa zao na mabinti. Hasa kama wake
zao wameshazaa. Huu ni unyama huu".
"Kwa hiyo....?" Mume akauliza.
"Kwahiyo me naogopa sana. Naogopa labda umeanza au ukaanza kufanya
mapenzi na hao mabinti wabichi. Mimi nimezaa sipo kama nilivyokua binti mbichi.
Angalia maziwa yangu yamelala, tumbo linakovu la operation. Me siwezi
kushindana na hao mabinti wa mjini naogopa watakuteka kabisa na ukaisahau
familia yako.." Mke akaongea huku akionesha wasi wasi.
Mume akaacha kufunga tai na akamtazama mkewe usoni. Akatabasamu. Then
akaanza kuongea
"Naanza na namba Moja, huwa nashangaa hizi takwimu zinatoka wapi.
Asilimia 52? Sijawahi kuwaza hilo. Hiyo asilimia 52 isikubabaishe mpenzi
wangu.. cha msingi ni kuamini maneno yangu".
Akaanza kumfuata mkewe alipo.
"Namba mbili, mimi sio mnyama. Mimi ni mume wako. Uliolewa na mimi
sio kwa sababu mimi ni mnyama lakini ni kwa sababu uliniona ni KING na
nastahili himaya yako. Sijaumbiwa roho ya unyama bali ni kwa nguvu ya roho
mtakatifu. Ninaishi kwa principles.."
Akasogea zaidi kwa mkewe na kumbusu kwenye paji la uso.. kisha
akaendelea...
"Namba Tatu, ni kweli kabisa hauwezi kushindana na mabinti wa
mjini, Usijaribu wala usithubutu kushindana nao maana hawapo kwenye ligi yako
na hawataifikia. Hawawezi hata kujifananisha na wewe, hawawezi kuvaa viatu
vyako, busara na hazina ya maarifa yako
hawawezi kufikia.
Haujaishi maisha yako basi, bali umeishi maisha yako na mimi. Hawana
kumbukumbu na expirience ambazo mimi na wewe tumezipitia kwa pamoja. Hawataweza
kuni-handle tabia zangu kama wewe unavyoni-handle. Sana sana watataka pesa
zangu na watakuwa tayari kufanya lolote kwa minajili ya kunila pesa zangu..
kimsingi hawana hata thamani ya kujifananisha na wewe malikia wangu.
Akachukua simu kutoka mkononi mwa mkewe na kuiweka kwenye meza...
"Kuhusu maziwa yako. Kila siku ya Mungu inapokwenda maziwa yako
yanakua mazuri. Maziwa ni maziwa lakini
yako ni mali ya mwanamke naempenda" Mume akaongea huku akiyashika taratibu
taratibu. Mke akatetemeka kwa mshtuko
"Maziwa haya umenyonyesha wanangu kwa upendo wa mama usio na
kifani.... kwanini nisiyapende?
"Tumbo lako, unasema lina kovu, me naliona liko sexy... limekua
nyumba ya wanangu. Uliwabeba kwa upendo mkubwa.. nilifurahi kuligusa pale
ulipokua mjamzito.. hata hivi sasa nafurahi kulishika.
Kovu la operation. Hili linanikumbusha madhila uliyopitia, hii
inanifanya nikupende zaidi.."
"Miguu yako.. imetembea na mimi kwa kila hatua hata pale tulipokua
hatuna usafiri tulitembea kwa miguu pamoja. Uliniamimi pale nilipokua sina
kitu, miguu yako ikasimama na mimi na ukanitia moyo. Mpaka kufikia hatua hii
tukiwa na mali za kutosha ni mchango wako mkubwa sana...
"My love, wewe bado ni namba moja. Hakuna mwanamke aliye mkubwa
kuliko wewe au mdogo kuliko wewe ambaye yupo kama wewe na atakaeifikia ligi
yako. Hawana viwango vya kukufikia. Mimi ni mfalme kwa malikia mmoja tu.
Malikia huyo ni wewe"
Mke akavua night dress yake.. akamkumbatia mmewe na kumbusu kwa hisia
kali, alimhitaji mumewe.. alimhitaji ampe raha kusindikizia maneno mazuri
aliyoyasikia kutoka kwenye kinywa cha mumewe mpenzi.
Mume hakufanya makosa.. akajisogeza na kuangukia kitandani and they
made passionate love ile asubuhi.. the kind of love that foreigners cannot
intrude.
Aliye mfalme huilinda himaya yake isiingiliwe na wevi...
Mwenyezi Mungu aiponye ndoa yako na kuiimarisha kwa pale penye kila
dalili ya kuleta mtafuruku ...
That man is me hutaki sikulazimishi ila mke ndo sijapata. 😜😜😜😜😜😜.
Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment