Sehemu Ya (7) : Naulizwa WHY GIRLS?? Kwanini Nawaandika Sana.
Jibu ni rahisi sana,Wanawake ndio vichwa vya nyumba
kivuli.... Baba ni kama Rais lakini MAMA ni Waziri Mkuu... Mtendaji mkuu wa day
to day activities za Home Government... Waziri mkuu feki ni hasara kwa nyumba..
Lazima washibe neno haswa ili hiyo nyumba isimame. Baba bila Mama bora hakuna
Familia....
I have a lot to share to girls, natamani Familia Bora sana
kwenye Kizazi hiki cha Nyoka aisee, na sitoacha mpaka nione Ma-mama bora
wakizaliwa huku mitaani....
Leo nna katopic tena kwa ajili yenu, Wanawake... Najua siku
hizi mmepata Hobby Mpya.... KUPENDA NDOA!
Hii Hobby inawacost sana maana hamu zimezidi uwezo....
Mnatamani sana ndoa lakini uwezo na credits za kuipata HAMNA... Sasa miujiza
hii ya Maji kugeuka Divai mara ya mwisho alifanya Yesu tu kule Kana ya
Galilaya, sijasikia tena maji kugeuka Ndovu Tandale... You must work for it...
Very hard...
Na jinsi gani unaweza kuwork... ni discpline tu... Manage ur
attitude! Wengi wenu ni kama mshakata tamaa... Mnajiendesha tu kama Guta...
Values za Mapenzi hamna tena... Miiko ya Mapenzi mnaivunja bila hofu... Mapenzi
yamekuwa Useless, kwahiyo kwenu lolote ni sawa.... SI SAWA!
Kuna tabia ambazo, kama wewe ni Mwanamke na unazo, SAHAU
kwamba utakuwa mke wa mtu, labda huyo atakayekuoa awe Stevie Wonder...
Namaanisha kipofu, poyoyo, hakujui amekurupuka tu.. Maana Wanaume hao wapo pia
wanadamka tu na kuzama dimbwini kisa Housing.... Kaona una shape kajaa kimiani,
kumbe angelijua..... Ange... ishakula kwake anajitia kitanzini!
Kati ya Tabia ambazo Wanawake wa Kizazi hiki wanazo, na
hawajali, bila kujua zinawaharibia Pozi kinoma, na zinawapa kitu wao wanaita
Gundu, kumbe Gundu wamelikumbatia wenyewe, na wanalisababisha wenyewe ni hizi
hapa:
1.MWANAMKE SAJENTI WA JWTZ MAKUTUPORA.
Tunawafahamu Wanajeshi.. lugha yao nzuri na tamu ni AMRI....
Lete... Kuja... Kwenda.... Rudi... Sasa Mwanamke tangu lini una Amri kama umekabidhiwa Kombania
ya JKT??? Mwanamke yake mapozi na politeness... Lugha tamu.... Mwanaume
hahitaji Amri maana nature yake ni amri tosha... Akumbane na Amri za Bosi wake,
na wewe home umletee Amri. Sasa nani BABA??.. KINANUKA FASTA!
Utawasikia, We Papito Casto hivi huoni kwamba sina viatu?? We Kataza, si nimekwambia Sina Vocha???
Lugha nzuri zimejaa teleeee... Baby wangu sina vocha ai
weweeeee, nitumie japo buku. Unamrembea mkaka Sauti, HACHOMOKI!.... Mwanaume
ukishamrembea sauti hivi hata kama hakuwa na mpango atanunua tena Buku 2
atatuma tu.... Sasa wewe endekeza Amri uone, utabip weee, utaishia kuomba TIGO
NIWEZESHE!
2.MWANAMKE USELESS.
Role kuu ya Mwanamke ni USAIDIZI.... HELPER.... Hii ni
Kibiblia kabisa, Mungu akaona si vema Adam awe peke yake, akamtafutia
Msaidizi.... Sasa wewe Mwanamke husaidii anything, badili tu jinsia yako! Kama kuna jambo moja tu unaloweza kunyonga Hisia za Mwanaume
na akakupenda maisha yake yote ni kama utatimiza hili jukumu vizuri....
Kuna watu mnakaa na Boyfriends wenu/Wachumba/Waume, hamjui
anafanya nini... Ana wazo lolote la Kibiashara... Humsaidii kumpa Mawazo mfanye
nini kuongeza Kipato.... Sasa we wa nini kwenye Maisha yake???? USELESS
Akitokea Shankupe anayejua hii Siri anamuiba fasta,
utashangaa, Huyu Mwanaume kafuata nini pale kwa yule shosti hata Sura hana,
NDIO, Sura hana,Shape Sony Wega ya Inchi 26 kama Mjapenga lakini ROLE KUU
kapata 100% kwanini jamaa asikutose???? Inakula kwako I guarantee.
Likikugusa badilika...Onyesha kwamba upo.. Show ur
presence... Mwanaume kila akikaa akihesabu Mafanikio anakuona upo behind this..
Behind That.. behind that and that one.... Sasa kila kitu kafanya mwenyewe,
hela hujachangia... Hata wazo??? Come on Girls!!! You can do better than that.
3.MWANAMKE DEBIT AND CREDIT NEVER.
Hawa ndo Kiboko yao! Hakuna wazo atakalokupa ambalo ni la
kuingiza hela.. yeye kila wazo lake ni la kupulusa kilichopo bila kujali
kitarudije na zikiisha itakuwaje! Wanatumia ile 'Shauri yake Principle' Baby twende Maisha Club Leo kuna Usiku wa Mabeste anazindua
Album jamani, Nampenda kweli Ben Paul atapafomu....
''Baby uko Mlimani City?? please nichukulie 'Tuna' Fish hapo
njaa inauma kweli mpenzi.. hata hujui ana hela au hana, kiruu!
''Baby, nimeona cheni nzuri kweli can i have 60 thou mpenzi
wangu, mwaahh... Ulimpa hiyo 60 thou?? Ilikuwa kwenye Plan??? Is it necessary
ununue leo???? THINK!
''Honey, kuna Samsung Galaxy nzuriiiii nimeona dukani, kama
ile ya BFF wangu Joanita''
''Mpenzi,bhivi huwezi hata kuninunulia VITZ,bkwakweli
nimechoka Daladala''.....bUmechoka daladala wakati mamako bado anapanda, tena
za Tandika... acheni biashara kichaa, hailipi!
Sisemi usiombe hela au vitu lakini hakuna hata sentensi moja
ambayo ni Income Generating inaweza kutoa kinywani mwako hata mara moja kwa
mwaka ili huyu MKAKA akumbuke kwamba She did this last year???? Hata kusema mpenzi nimeona tangazo kiwanja kinauzwa can we
go see it and buy tujenge when tukioana?? Au Mpenzi kuna this Business nimeona
rafiki yangu amefanya inamlipa sana, can you think of doing it???
Wewe ni Debit Debit Mwanzo Mwisho, hakuna Positive hata
moja??? Halafu unataka huyu jamaa A-propose ndoa??? Na unamkomalia kwamba mbona
yuko kimya hasemi kitu mwaka wa 3 huu??? Apropose kuoa DEBIT???? Ah nani
kasema, utasubiria Treni hapo Ferry, subiri hapo hapo hadi usikie honi..
Anakutafutia tu Timing ya kukumwaga, maana ur a Liability to him japo
hakwambii!
4.MWANAMKE CHAUPEPO.
Hawa kama ni graph basi inaongezeka huku ikiongezeka...
Waingereza wanasema Increasing in Increasing Rate! VYAUPEPO!
Jumatatu yuko Samaki Samaki...
Jumanne yuko Club Rouge...
Jumatano yuko New Palm Bar kwenye Baikoko na Friends.....
Alhamisi yuko Ladies Free Billicanas...
Ijumaa yuko Elements....
Jumamosi yuko Runway.....
Jumapili yuko Skylite Band Thai Village.....
Ana Ratiba kama Mbunge wa Msovero! Unajua kuna mambo Wanaume wanafanya, sawa, ila Wanawake
mkiiga wala haifai... mtasema mbona Wanaume wanafanya, lakini ukweli unabakia
palepale, Mwanamke Chaupepo wa usiku ana-raise lots of Question Marks...
Lots.....
Mama wa nyumba ajaye, anapepea haifai, hata Bendera ya
Mwenyekiti wa Kijiji haikufikii, Wiki nzima una mishe, hujali hela ngapi
umetumia kama kweli ni za kwako unajitegemea, but it shows that HUNA FOCUS....
Na hili lina-apply hata kwa Wanaume, siku 4 kwa Wiki zote
unatoka, hata kama unatumia 20thou kwa siku, still its too much... ukisave hiyo
hela unanunua tofali za kutosha tu.... Mtalalamika ujenzi shida lakini hela
unazokula gambe ili bata ikuzoee ukiichange FOCUS yako kidogo utashangaa
kibanda kinainuka taratibu... Siongei Rocket Science, inawezekana, Nimeona na
ninazidi kuona.... Change ur focus and things around you will change... MEN,
HEAR THIS!
5.MWANAMKE ZEZETA/GOIGOI/KILAZA.
Mwanamke lazima awe Sharp... Bed... Jikoni... Everywhere!
Make your Man proud of YOU!! Ukiwa Sharp hata mmeo atakusifia kwa rafiki zake,
hiyo kafanya mama flani bwana.... Sasa mmeo hana hata kimoja cha kukusifia....
Bed pia uko shallow na you dont bother kujifunza wala, unaona utaaaammmm... Mh
mama, wataka ndoa ama ndoano???
Mkisoma Sifa za Mke mwema kwenye Biblia ndo mtajua.... Mke
sio Sura au Shape, hata Punda ana shape... Mke shurti uwe SHARP..... Kuna nyumba ukiingia tu unajua Mke KILAZA... liko wazi....
Mwanamke Sharp hata ukifika kwake utaona.... iko clear na kilaza iko clear...
Kuna watu wanaoa vilaza wanajuta... Mke hajui kupika, kutwa
alikuwa anashinda vibanda vya chips na kula burger... Kisa ana shape umeweka
ndani, dadeki bonge la pancha, muda wote anatengeneza kucha... Mwanamke kufua
hawezi/hataki eti ataharibu kucha.... Mwanamke anajua Kuoga na Kuvaa tu.... Mwanamke
kupika hawezi anamuachia Housegirl kila kitu.... mahausigeli siku hizi ukizubaa
tu MESSI huyooooo kapita, unapinduliwa Uganda hivihivi na IDD AMIN upo
hapohapo!
Mwanamke kitanda akutandikie Housegirl???? Halafu unategemea
nini??? Kama Housegirl anashine in the eyes of your Man kwamba yeye ndo
Masterplanner wa House, Mmeo atajuta kwanini alikuoa wewe ni afadhali
angem-turn Housegirl into a Wife....
Tafadhali, Think Twice, Ndoa sio kama Vinyweleo kila mtu
anavyo... Zile Zama zimepita.... Utabakia kutegesha Mimba huolewi Ng'o maana
huoleki...
Kama una hizi Tabia BADILIKA lasivyo chagua, ama UJIOE au
UOLEWE na Same type of Stupid Man as ur maana mtakutana wote level za Ngassa na
TEgete...ASANTE.
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment