Sehemu Ya (55) : Siku Zoote Usifanye Maamuzi Ukiwa Ndo Kwanza Umefall In Love.


Wahenga walisema usifanye maamuzi ukiwa umefurahi sana, au ukiwa una
hasira sana... Mimi naongeza, Usifanye maamuzi ukiwa ndo umefall in Love.. Bado una kimuhemuhe cha kuanza mahaba na mtu, watu wengi huwa wanakosea hapa...

Kuna watu imewacost... Anaanza Uhusiano na mtu eti kuonyeshana wanapendana anampa ATM na Password.... Mwingine eti anafungua Joint Account.... Na Boyfriend??? Girlfriend??? Chonde...

Wengine wanajifanya wako very focussed, wanafungua Biashara ya Pamoja, wanachanga kimya kimya wakiwa wamejifungia chumbani na Mishumaa, wanaanza biashara ya mbao pamoja, haijaandikishwa popote... 

Nguvu ya Mahaba.... Kimbembe baada ya miezi miwili, mambo hayaendi, sikilizia balaa lake.. Naomba ATM yangu nakwambia, mbona umedraw hela zangu hujasema, rudisha, ntakufunga nakwambia... Ulipaswa uwaze, How do u give Boyfriend mmekutana wiki 2 ur passwords za benki... so sensitive... acha kuwa na akili za uji wa ulezi, use ur brain.. sio unatekwa tu na Mahaba mpaka unafanya vitu bila kuwaza... Si kila Girlfriend anakuja kwao kwa wema, wengine wameona una vitu, we unajifanya uko dimbwini unampa ATM anakukamua mapene yote.... 

Si kila Mwanaume ana mapenzi, ukijifanya we mtaalamu wa kufall unampa tu vitu, siku akikugeuka huna pa kushika maana vyote alivyokupa mlipeana Kitandani mkiwa mshapimana ubavu na mijasho lundo... Use ur brain acha kujifanya we penda penda, Ubwege huo utaliwa siku si nyingi, Mapenzi yenyewe yako wapi siku hizi, wizi tu.

Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter ,@KissToTheLadies 

WhatsApp +255 715 758 021

No comments