Sehemu Ya (49) : Kinawatofautisha Wanaume Na Wanawake Kwenye Mapenzi.


Kinachowatoufatisha Wanaume na Wanawake kwenye Mapenzi ni jinsi gani ya
kutumia HISIA na AKILI katika Kubalance Mapenzi!

Wanawake wana tabia ya kuzama Dimbwini kama Perege ameona tope, yaani wanazama mpaka wanasahau wana kichwa chenye Akili ambazo anapaswa pia kukitumia katika REASONING... Unakuta Demu anafanyiwa vitu Obvious kabisa na Mwanaume anaye date nae lakini yupo tu na ukimuuliza anajibu kibwege kabisa, ''I loove him jamaniii, najitahidi nimsahau nashindwa', unamuangalia unatamani umuwashe makofi..

Ukifall In Love usitumie Hisia tu, Beba na akili yako muende Pamoja... Itakusaidia Sana! Pale Hisia zinapokufa Solution za Kibwege Akili yako itakusaidia kukwambia kwamba Unapoteza Muda na unapaswa kuchukua hatua! Akili inasaidia kukupa alarm ya kila kinachoendelea kwenye Penzi lako wakati hisia inafukia tu mashimo na kukutia moyo eti mambo yatabadilika. UJINGA!

Wanaume wana uwezo wa kuutumia Ujinga wa Hisia zako za Division 5 kukuaminisha kwamba Ur the Only One for him, wakati Akili ina uwezo wa kuvumbua kwamba kwenye Moyo wake mmejazwa wengi kama Foleni ya wagonjwa wa TB.

Fall kwa Hisia lakini Beba na Akili zako, Hutafanywa Mjinga hata kwa Sekunde.

Kwa Hisani ya Wanaume wote waliozama Dimbwini Kwa Hisia Tani 20,000 na Akili Terrabytes 5000.

Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter ,@KissToTheLadies 

WhatsApp +255 715 758 021

No comments