Sehemu Ya (48) : Mghiniii Usipokuwa Na Hela Watoto Wazurii Woote Taishia Kuwaita Shemeji.
Huu ni Ujumbe kwa Wanaume wenzangu popote mlipo... Uanaume
sio mchezo. Tafuteni Pesa Usiku na Mchana.
Ukiona Kila Mdada Mzuri unayejaribu kujisogeza-sogeza kwake
ili baadae uweze kujiweka awe wako haoneshi dalili ya ku-respond na hata
aki-respond basi atakuwa anakuita majina ambayo yanakupa Alarm tu kwamba
NETWORK NOT REACHABLE HERE jua wallet yako ina Pancha!
Mtu unamuonyesha kabisa unampenda halafu yeye anakuita SHEM
WANGU, SHEM AKE, SHEM JEMBE, SHEM LAKE MIE, SHEM BOO BOO... Sasa ukishaitwa
Shem ndo imekula kwako, humpati hata kwa kikombe cha babu wa Loliondo.
Ukiona Msichana unampenda na anajua kabisa unachotaka halafu
anakubandika jina SHEM SHEM ujue ndugu yangu huna Hela, Kemea kabisa Pepo la
kuitwa Shemeji!
Wahenga wa Siku hizi wanasema, UKIWA HUNA HELA, WASICHANA
WOOOTE WAZURI WATAISHIA KUKUITA SHEMEJI.
Ukitaka kuitwa Baby na huna hela, nenda kijijini kaoe huko
utawapata wenye magaga, mjini kila Msichana mzuri ana Price Tag kama nguo za MR
PRICE. Mashemeji mpoo???
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter ,@KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment