Sehemu Ya (50) : Kumfurahisha Mtu Mwingine Zaidi Unavojifurahisha Nafsi Yako Ni Kujikosea Adabu.


Jipende kwanza wewe kabla hujajitoa Kimasomaso na Kimuhemuhe chako cha
Mahaba na kujibeba mzobemzobe na kuubwaga moyo wako mwaaaaaaaah chini
kwa mtu mwingine kwa Mahaba shanta shanta halafu huyo unayedhani anastahili kupendwa kuliko unavyojipenda anaishia kuumwagia moyo wako Tindikali mchana wa Jua kali!

Wengi mnaumizwa kwa sababu mnawapa watu wengine nafasi kuuuubwaaaaa kwenye mioyo yenu mkidhani wana miujiza na watatibu maradhi yenu ya moyo kwa Mwarobaini... Jamaa wakizingua mnaumia nusura kukata roho. JIPENDE KWANZA

Ujue wazi kujisumbua kumfurahisha mtu mwingine zaidi ya unavyojifurahisha nafsi yako ni kujikosea adabu na kujinyima kusiko na akili... Bila yeye pia unaweza kuishi, unaweza kuenjoy maisha, unaweza kusmile.. Furaha yako haiko kwenye Remote ya Mwanaume/Mwanamke mwingine
Kutegemea mtu mwingine akupe Furaha utasubiri sana, Dunia imejaa Heart Breakers tu, wako kila kona, kila unayempa moyo ana gudulia la Tindikali, ananyunyizia tu kama anamwagilizia mbolea ya DDT kwenye Mahindi.. UTALIA KILA SIKU.

Kujipenda ni Rahisi sana, Jipe Raha, Ukisubiri Kupendwa dunia ya leo ni ngumu kama kumfikisha kileleni Changudoa wa Corner Bar, labda utumie mwiko... Love Yourself First, Ukipendwa iwe BONUS tu.


Kwa Hisani ya Wanaume wote mlio Dimbwini bila Vigudulia vya Tindikali mkononi.

Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter ,@KissToTheLadies 

WhatsApp +255 715 758 021

No comments