Sehemu Ya (47) : Sura Huna Hela Pia Huna.. Basi Ukisitiriwa Ujue Kusitirika Jamaani.
Ukipewa Msaada wa kubebwa mgongoni, usianze machejo ya
kumtekenya aliyekubeba, atakuangusha bure..
Hii ni kwa wale WANAUME wasio na Shukrani.. Unajijua kabisa
huna Mvuto na Sura yako haina haiba, kwa kifupi una Sura Kama Yangu kama bata
mwenye mdondo lakini Mungu sio Mrisho Ngasa, kuna mdada wa watu bila kujali
muonekano wako hafifu na duni, amejitoa Kimasomaso kukupenda kwa dhati japo
huna Sura wala huna hela na hadhi ya kuwa na msichana kama huyo.
Mdada wa watu
anajitahidi kujilinda, anakwepa vishawishi vya Mapedeshee wa town ambao
wanahonga kuliko kutoa sadaka kanisani, anakataa Ma-handsome boy kibao
wanaomtaka, kwa sababu yako. Badala ya kushukuru na kulipa wema, angalau na
wewe anakuweka mjini unaonekana unamiliki mzigo wa maana, unaonekana nawe umo
wewe ndo umekuwa Fungulia-Mbwa, Unamcheat wazi wazi.
Sasa hivi unajiona mjanja kwa sababu yupo, na unajua
anakupenda ila siku moja atakuchoka atakuacha, Sasa Sijui utapata wapi mdada
mwingine wa kujitoa Mhanga kukupenda na sura lako kama umepewa taarifa ya
Msiba.
Heshimuni Wadada wa watu wakijitoa kuwapenda kama mlivyo...
Nakushangaa sana wewe Kijana unapata wapi Ujasiri wa kuleta mawenge kwa huyo
mdada wakati unajua kabisa Hela huna na una sura kama Bonde la Ufa.....
UKISITIRIWA BASI UJUE KUSITIRIKA.
Kwa Hisani ya wangoni waishio Dar.
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter : @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment