Sehemu Ya (46) : Ukiwa "Mchaga" Wa Mapenzi Biashara Ya Mapenzi Haitakusumbua.
Mapenzi hayana tofauti na Biashara ya Duka, Bahati mbaya tu
Mapenzi hayana Kabila. Laiti Mapenzi yangekuwa na Kabila basi Wachaga wangekuwa
wanafaidi
sana Mapenzi maana wana Discpline sana ya Biashara... Wachaga wana
uwezo wa kugeuza Genge likawa Duka.. Na Duka likawa Supermarket... Na
Supermarket ikazaa Hoteli... wamenyimwa Miguu tu bahati mbaya wakapewa Fito
lakini unene wa miguu yao Mungu amewapa akili nene za kibiashara (semeni Asante
sio dongo)
Kanuni ya Biashara ni Kuheshimu Mtaji na Kukuza Mtaji ili
upate Faida zaidi Biashara ikue... Haijalishi kama Mtaji wako ni Mdogo,
Ukiuheshimu utakutoa
Penzi likiwa Dogo liheshimu.. Ile miezi ya mwanzo mkiwa bado
mna Penzi la Vibration ndio Muda wa kukusanya Mtaji wenu wa baadae. Mkishindwa
kukusanya Mtaji kwenye kipindi cha BOOM kile mkiwa bado mna masham sham,
unatoka Bunju kwenda Kibaha kupewa tu Goodnite Kiss basi biashara itawashinda
muda wa SLUMP wakati tunutu wameshaanza kuingilia penzi lenu na ubize usio na
maana...
Huwezi kutumia Mchele wa dukani kupikia Pilau wakwe wakija Home
kukusalimu, Biashara na Familia havina uhusiano
Ukiwa Mchaga wa Mapenzi Biashara ya Mapenzi haitakusumbua
maana utajua ufanye nini kwa wakati gani ili Graph ya Penzi lenu iendelee kuwa
juu daima. Mchaga hafanyi Shopping ya Jeans Mpya mwaka mzima ili Duka likue...
Sacrifice kwenye Mapenzi ni LAZIMA kama unataka Penzi lenu libaki juu, Ukiogopa
kuwa bwege wa Mapenzi duka lako la Mahaba halitakua.
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter ,@KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment