Sehemu Ya (42) : Mapenzi Siku Hizi Hayana Tofauti Saana Na Mitandao Ya Simu.


Mapenzi hayana tofauti na Mitandao ya Simu... Wanatumia gharama kubwa sana kujitangaza na kuwapata wateja... Wakiwapata wanahakikisha wateja wao
wanaridhika na Huduma na wanabaki kutumia Mtandao huo mmoja tu na bila KUHAMIA kwenye mtandao mwingine.

Usione Tigo wajinga wanapohakikisha wateja wao hawahamii Airtel kwa gharama yoyote na ndio maana BABA LAO wakiongeza Dakika za kupiga Bure na Tigo wanaongeza kesho yake... A SATISFIED CUSTOMER becomes a LOYAL CUSTOMER.

Mapenzi hayachezi mbali na Principle za Mitandao ya Simu.... Ukitaka Usigongewe Demu wako INVEST kumfanya Demu wako awe SATISFIED... Mpe vitu vyote ambavyo Demu wako anastahili kupewa ili asiwe Machepele na Macho Juu-Juu... Mfanye asihisi kuna kitu anamiss kutoka kwako kumfanya atazame pembeni... 

Prove kwake kwamba wewe ndio Best of the Best na Unampa huduma Best na hahitaji mwingine... Mwanamke halindwi wala hawekewi Alarm, anajilinda pale tu unapompa sababu ya yeye kutotazama nje kuona kama kuna hali nzuri kuliko hali unayompa wewe.... Usipompa, Wanaume wenzio wa nje wataona hiyo Opportunity na wataitumia ipasavyo kuprove kwamba umefeli na wao wanaweza kumpa.

Usipompa Demu wako KABANG ya Kutosha atahamia CHEKA BOMBASTIK na Usimlaumu, ulikuwa na muda hukufanya, acha wanaojua wampe... Ukimuweka demu jangwani hakikisha yeye ni Ngamia au una maji ya kutosha kumkata Kiu. Kwa Hisani ya Wanaume wote walio dimbwini!.


Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter ,@KissToTheLadies 

WhatsApp +255 715 758 021



No comments