Sehemu Ya (40) : Maisha Yamefundisha Watu Kwamba Uzuri Wa Nje Si Mali Kitu.


Ukiona mtu kachumbiwa na anaolewa na Mtu ana Sura ngumu kama Physics usimcheke wala kumshangaa kwanini au amekosa nini hadi amkubali yule
mtu...
Watu wazuri wanatesa nyie... Wanaringa... Kwa sababu wanajua hata akikupoteza wewe leo kesho anakamata Danga jipyaaa na ngoma inasonga... Ila hawa wenye sura chachu wana heshima maana wanajua kikinuka, mpaka afanye Scrub Miezi 6 ndo anaambiwa I love you too 2...

Maisha yamefundisha watu kwamba Uzuri wa Nje si mali kitu, anaweza kuwa ana mvuto, Ukipiga nae Picha Photopoint Mashallah, Ukimuweka Instagram watu wanahaha, lakini anakuhenyesha na huna raha, wiki hii unamfumania Baa, wiki ijayo wake wenza wake wanakuchangia wanakudunda... Kisa cha kuishi kwa Presha??

Sasa wewe endelea kuchagua Uzuri wa nje, wenzio wanaolewa wewe unabakia kuongeza listi tu, Kamata danga Chee la ukweli, sawa watakucheka umeoa Mdada ana Sura kama kamwagiwa Tindikali lakini anakupenda kwa dhati kwa asilimia 100%


SURA HATA KONOKONO ANAYO.

Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Twitter @KissToTheLadies 

WhatsApp +255 715 758 021

No comments