Sehemu Ya (39) : Hakikisha Moyo Wako Una Free Space Kupokea Gigabytes Za Penzi Jipya.
Usiingie kwenye Uhusiano Mpya na Mtu mwingine kama unajua
kwamba bado Hisia zako na Moyo wako unampenda bado yule uliyemuacha na bado
anakumiliki theoretically na hauko tayari kuachilia Moyo wako kwa Mtu Mpya.
anakumiliki theoretically na hauko tayari kuachilia Moyo wako kwa Mtu Mpya.
Mwenzio huyu Mpya atajitoa kwa moyo wote akijua wote mko
safari moja kihisia kumbe wewe umeamua kwa Makusudi Kumgeuza Mwenzio HEDEX,
Unaingia mahusiano na Mtu ili awe kitulizo cha Maumivu wakati unajua kabisa
unaumwa TYPHOID.
Tafuta kwanza Dawa ya TYPHOID unayoumwa, Uwe tayari kusahau
yaliyopita na uingie penzi jipya ukiwa una moyo mpya ili upokee Penzi Jipya...
Lasivyo utamsumbua Mpenzi wako Mpya anajitahidi Kukupa HEDEX kutibu Typhoid na
wewe umekaa kimya humwambii kwamba anatibu ugonjwa asioujua.
Format your Heart, Hakikisha Hard Drive yako ina Free Space
kupokea Gigabytes mpya za Penzi jipya na sio unakuja na Diskette halafu
unamkazania jamaa acopy Muvi kwenye Diskette...
Kama hauko tayari kwa penzi jipya jipe mapumziko kwanza ujue
unataka nini, Usitegemee Gari liende mbele wakati umeweka Gia ya Rivas.
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment