Sehemu Ya (37) : Mwanamke Aliye Kwenye Penzi La JKT Kukucheat Wewe Ni Rahisi Tu.


Wanafunzi wa form 6 waliposikia kuna kwenda JKT walifadhaika sana... walitamani iwe ndoto.. maana wanajua Jeshi Sio mchezo... Hakuna
anayependa jeshi, hata Mwanajeshi mwenyewe kuna nyakati anatamani apumzike..

WANAUME: Moja ya sababu kwa nini Wanawake wanacheat ni kwa sababu tunawatreat kama tuko Jeshini... Maisha ya Amri... Kukosa Uhuru... Kununa... Msiishi na Mademu/Wachumba zenu kama Mko Kambi ya Jeshi... Ni rahisi kujua mtu na demu wake wakitembea njiani, we angalia sura zao... Angalia ukaribu wao wanapotembea... Angalia mapozi yao wanapoongea... Utajua tu kama wako kambini au Lah... Mwanamke aliye kwenye penzi la JKT kukucheat wewe ni rahisi tu... 

Akikutana na Mwanaume Polite and Romantic (hata kama anapretend), ambaye anamsikiliza na kumpa uhuru, ujue imekula kwako... Na atakusaliti sio kwa sababu hakupendi, ila ni kwa sbaabu anapata Treatment ambayo kwako wewe Mjeda ni ndoto.

Mfanye demu wako atabasamu.. Mfanye awe na uhuru wa kukutania... Mfanye ajisikie huru akiwa na wewe... Ndo maana mademu wenu wana miaka 24 lakini sura kama Maajuza, umejigeuza Kanali na demu wako ni Kuruta, hamtafika mbali


Shkamooni wanaume wote wenye tabia za Kambi ya Jeshi Lugalo... TUBADILIKE.

Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Twitter @KissToTheLadies 

WhatsApp +255 715 758 021

No comments