Sehemu Ya (36) : Kuna Mtu Analetwa Kwenye Maisha Yako Ili Tu Aku Shape Kwa Ajili Ya Your Future Hubby / Wifey.


Kabla hujafall In Love ukazama na miguu kabisa muulize Mungu kwanza ''Huyu mtu aliyekuja maishani mwangu sasa amekuja kwa kusudi gani'??
Sio kila anayekuja kuwa Mpenzi wako wewe unamtreat kama Mme/Mke, siku akiondoka unapata vidonda vya tumbo, unalia kamasi debe 3 na kuanza kusema ''Why Me Lord'', nimejitoa sana kwake siamini we are not together, na kujiapiza hutapenda tena...

Kila mtu anayeletwa kwenye maisha yako analetwa kwa kusudi maalumu.. Mwingine analetwa kwenye maisha yako ili akufundishe Usafi na Kuoga mara 3 kutwa, hana sifa hata moja ya kuwa mkeo, we unang'ang'ana Mungu nipe huyu huyu... Mwingine analetwa akufundishe kuvaa soksi tu, we unataka abaki mfunge ndoa.. Mambo hayaendi hivyo...


Sio kila aliye mpenzi wako sasa ATAKUOA, wengine wameletwa wakushape ili Mmeo/Mkeo akukute umekaa mkao wa kuwa Mwanandoa... Usimpe jukumu lisilo Lake.


Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Twitter @KissToTheLadies 

WhatsApp +255 715 758 021

No comments