Sehemu Ya (30) : Je, "Ndoa" Itaendeshwa Na Makalio?? Nauliza.?
Umeumbwa vizuri kwelikweli, ukitembea unanata kama umepigwa shoti na umeme wa Songas.. Una sura.. shape mashallah na guu la bia ila akili huna.. na hapo ndo balaa lako lilipolala... Kila siku una-
upload picha kwenye Instagram, umependeza mwenyewe, uko kwenye Kitchen Party za mashosti.. Send Off na Harusi za mashoga zako mliosoma wote...
Nikiwaangalia wale mashosti zako walioolewa, kimuonekano umewazidi sana, by far, na wengine wana sura za Wajomba zao na shape za sanamu la Michellin.. Ila ndo wameolewa hao, wanapepea na waume zao.. we upo tu na uzuri wako.. utachangia sana harusi za wenzio na kujaza Instagram kwa mapicha ya minuso utadhani umekuwa Blogger msaidizi wa BLOG - ya Xxlbongotz .
Una miaka 30 na ushee, karibu hata hizo Make Up zinazokusitiri zitaanza kudunda usoni maana ushajisiliba kila urembo uliopo duniani na mume hupati... Wanaume hawaoi Uzuri na Urembo wa nje, Wanawake mjue hili... Wanaume wanaoa AKILI YAKO.. REASONING ABILITY YAKO... Sawa makalio unayo, yanavutia kwelikweli lakini Je, Ndoa itaendeshwa na Makalio??? J
IPANGE mtegemee mungu mlilie mungu wako piga magoti kwa uchungu atakuambia kwanini amekuumba na kwajili gani mungu atakusaidia atakupa wa kufanana na wewe uzuri bila hofu ya mungu Sawa na bure tusijisahau sana turudi kwa mungu.
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment