Sehemu Ya (22) : Usijifanye Una Mapenzi Ya Halmashauri Kupeleka Ripoti Kwa CAG.

Hivi Mwanaume anapopiga moyo konde akaja kukutongoza, jibu si unakuwa nalo mwenyewe??? Kwani anakuwa ametongoza ukoo mzima, au ndugu wote, au amemtongoza na Boyfriend wako kwa pamoja??


Kama jibu ni hapana mwambie tu, Am sorry siwezi kuwa na wewe coz nna Boyfriend tayari... Au sihitaji Boyfriend kwa sasa... Majibu yako mengi na unayo wewe uliyetongozwa! Simple. Sasa wewe unatongozwa, unaenda kumwambia Boyfriend wako, ohhh u know that guy Boownie?? Kanitongoza nimemkataa.... So what??

Ili uonekane ulielewa sana matumizi ya NO au unamuimpress nani?? Mbona wale uliowakubali hukumpelekea ripoti?? Usijifanye una Mapenzi ya Halmashauri kupeleka ripoti kwa CAG.

Ukitongozwa jibu unalo, ndo nyie mnafanya Wanaume wapigane visu ili mtafute ujiko kwamba fulani na fulani wamenigombania, we umekuwa Jimbo la Uchaguzi?


Kesi ya Nyani mmalizane nyani kwa nyani, mpe jibu nyani humtaki aende zake, ya nini kuwaalika Tumbili wawe mashahidi??? Eehbooh..

Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Twitter @KissToTheLadies 

WhatsApp +255 715 758 021

No comments