Sehemu Ya (15) : Jinsi Neno "Nakupenda Na Ntakuoa" Linavyo Wacost Ladies.
Ukinunua CD original ya Alicia Keys mtaa wa Tandamti
Kariakoo kwa Mmachinga aliyevaa Yebo yebo chafu za Zambarau, sitashangaa
ukifika nyumbani ukaiweka
kwenye deki ikaanza kuimba Shamukwale.Vitu viwili tofauti kabisa! Ni makosa yako, vitu Original
huuzwa sehemu special, sio mkononi kwa mmachinga...
Kuna wadada, na akili
zenu zote, unakutana na Mwanaume ameshaoa, ana mke na watoto wawili, anakwambia
anakupenda, yuko tayari kumuacha mkewe akuoe wewe, na wewe ulivyo na akili za
ubuyu unaona hilo ni zali.. Zali ni kwa mentali tu, huo ni upuuzi, na kama
unadhani huyo Mwanaume anakupenda umeula wa chuya.
Kama Mwanamke mwenzio
kajitahidi kukata viuno miaka yote na kapewa na pete, amegeuzwa kuwa Incubator
ya kutotoa watoto na kaachwa, wewe utafanya muujiza gani usiachwe siku moja
ukishatotoa pia?? THINK..
Kama ana uwezo wa kumuacha
mke wa ndoa kwa ajili yako, na kusahau viapo alivyoahidi mbele ya Kasisi na
Kadamnasi, unadhani ataogopa kukubutua mateke wewe??
Ladies, neno
'Nakupenda na Nitakuoa' yanawacost, mnapoteza utu wenu na kutoa mioyo yenu kwa
wagoloko wa ajabu.tumieni akili kufikiria Outcome ya jambo na sio kutumia Hips
kuwaza.
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment