Sehemu Ya (13) : Mpenzi Halindwi Kama Alarm, Watu Watai-Snooze Na Watamuiba Kama Kawa.


Mpe Mpenzi wako sababu ya yeye kujilinda akiwa mwenyewe hata kama haupo... Usitumie Nguvu na Ubabe kumlinda kama hana sababu ya yeye kujilinda mwenyewe. Mpende na ajue anapendwa ili asiwe na sababu ya kuuchakachua
upendo unaompa maana unamtosha kumlinda dhidi ya maupendo feki ya mtaani.


Sasa wewe badala ya ku-invest muda wako kumpa Upendo wa kutosha, umejigeuza Alarm, unadhani kwamba unaweza kumlinda asiibiwe au asikusaliti... Unapoteza muda kumfuatilia anaenda wapi, na nani, na kwanini hajaaga, unamfuatilia nani kamtumia meseji na nani anaongea nae kwa simu mpaka unaenda kuprint statement kwenye mtandao anaotumia... Unapoteza muda wako



Kama hujawahi kumiliki hata Shina la Mgomba utawezaje kumiliki mtu??? Mpenzi halindwi kama alarm, watu watai-Snooze na watamuiba kama kawa, Mpe sababu za kujiona anapendwa ili ajilinde mwenyewe. Kumlinda Mpenzi ni sawa na kulinda Bahari, wewe unalinda Coco Beach wenzio wanavua samaki Bagamoyo msipoteze nguvu nyingi kumsifia vitambi kwenye snap chat eti you like it wakati ukweli mnajua mnataka six packs huo ni Wizi... Msitupange tunataka uhuru wa kujilinda.


Pia Unaweza Nifollow:

Facebook , Instagram , Twitter @KissToTheLadies 

WhatsApp +255 715 758 021

No comments