Sehemu Ya (12) : Shikamoo Wanawake Wa Dar, Mnakata Kabla Ya Kona.
Wakati wewe ukienda Muhimbili kujisomea Miaka 7 ili uwe
Daktari Bingwa kuna wenzio wako Mtaani na Mtaa umewafanya wawe Madaktari huku
wakiichambua Biology kwa macho tu bila hata kwenda Shule..
Kuna Wanawake wana balaa utadhani wanatembea na Ramli ya
Mganga, usiombe awe ndo mchuchu wako Mtagombana deile, wanajifanya wanajua
kukagua kuliko maafisa wa TRA Makao Makuu.
Msipoonana wiki 2 mathalani umesafiri, ukirudi sasa ukafika
ule muda wa kupunga maruhani utamsikia, ''huko ulikoenda uliibiwa na nani?? Mbona
Jongoo amesinyaa hivi, Utanieleza nakwambia'', timbwili la haja, kumbe maskini
joto tu la Dar limesababisha Bunsen Burner imekuwa Non luminous Flame
Mtaishi maisha yote mtu mzima kama uko Laboratory, wana
maswali yao fyongo-fyongo tu, utasikia ''Mbona unanukia kama kile kisabuni cha
EVA cha gesti, leo umeamkia wapi??? Kubwa kuliko utaambiwa ''Leo uko tofauti
sana halafu hata kamshindo kako leo kana lita chache sana, mwanaume huridhiki
weye hata upewe kila siku''.. mmmh, yaani hadi lita wanapima kwa macho na
feeling, mweh
Kama wewe mtaalamu sana si ukasaidie kutafuta ndege ya
Malaysia iliyopotea?? Unahamishia Biology kwenye mahaba, watu hatupumui kwa
raha, unakaa wima-wima leo ntaambiwa kitu gani, hukawii kuambiwa mbona Lips
zako kavu hivi umetoka kumbusu nani.. khah... Utadhani umeoa Anthropologist
kumbe Banker tu!
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment