Sehemu Ya (160) : Mpenzi Aliyepoteza Ladha Katika Mahusiano Yake.. Utamjuaje??

_Siku zote huwa anataka yeye kuwa juu ya mumewe yani si mtu wa kujishusha
ktk kila jambo, kauli mbovu na sauti ya juu wakati akiwa anazungumza na mumewe hivyo ni vitu vya kawaida sana kwake, hana hofu juu ya ndoa yake yaani si wife material tena.

_Hupenda mabishano kwenye kila kitu, si mtu wa kupokea maagizo kutoka kwa mumewe na kuyafanyia kazi ipasavyo bila kubishana, anapemda kufanya argumentation kama  mbunge wa viti maalumu.

_Ni mtu wa kulalamika sana kwenye mazuri na mabaya, si mwepesi kushukuru kwa chochote kiwe kidogo au kikubwa, kila analotendewa kwake si jema hana kawaida ya kuridhika.

_Tendo la ndoa kwake ni kama adhabu ya push up, kumpa unyumba mumewe siku hiyo hadi majirani watajua kuwa leo mume anahitaji mzigo, hawezi kulifanya jukumu hilo kama wajibu wake ila hadi alizimishwe na mara pengine kumpangia mumewe ratiba siku za kukutana naye kimwili.

_Hajui kitu bahati mbaya, akili yake inamtuma kila analotendewa limedhamiriwa, yaani hakuna mistakes kwake, mumewe asikosee kitu.

_Mashindano kwake ni jambo la kawaida sana, mfano: mumewe akiwa busy na kazi asipomtumia msg au kumpigia basi na yeye hufanya vivyo  hivyo.

_Hupenda kumlinganisha  mumewe na wanaume zake waliopita (kumtoa kasoro) na marapengine hujuta kuolewa na mume alienaye na kuwaona waliokuwa wakimchezea ni bora zaidi ya mumewe.

Inawezakana ikawa ni kweli wanaume ndio wanaongoza kuvuruga ndoa zao. Ila je ulishawahi kujiuliza kwamba uwenda mwanaume wako anachepuka kutokana na kero zako.?

Ili ndoa iwe bora inahitaji amani na upendo, utulivu wa nafsi na upole kwa kila mmoja. Mwenyejukumu la kufanya ndoa iwe bora si mwanaume pekee ila hata wewe mwanamke pia ni mtu muhimu kuipigania ndoa yako kuwa ktk misingi imara.

Usipende kuishi kwa mazoea.

Jitathmini  Mwanamke.

Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Ili Kupata Posts Zangu Kirahisi Zaidi Kwenye Simu Yako.http://www62.zippyshare.com/d/FvrvpQQg/31722/xxlbongotz.apk
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies 
WhatsApp +255 715 758 021

1 comment:

  1. Ushuhuda

    Nilivunjika kabisa uhusiano wangu ulipoisha. Niliamini kweli nimepoteza upendo wa maisha yangu milele. Kisha nikampata Dk. Dawn, na kila kitu kilibadilika.
    Kwa fadhili, hekima, na mwongozo wenye nguvu, alinirudishia upendo ambao nilifikiri umetoweka. Leo, tuna furaha zaidi kuliko hapo awali!
    Dr. Dawn kweli aligeuza machozi yangu kuwa furaha.

    Dk. Dawn Anaweza Kukusaidia Na:

    ✅ Maneno ya mapenzi
    ✅ Tahadhari za Ujauzito
    ✅ Kurejesha Ndoa/Mahusiano
    ✅ Dawa za mitishamba kwa VVU, Ugonjwa wa Figo, Magonjwa ya Moyo, Maambukizi na mengine mengi.

    📧 Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
    📞 Simu/WhatsApp: +2349046229159

    Usiteseke kimya kimya. Dk. Dawn anaweza kurudisha furaha katika maisha yako!

    ReplyDelete