Sehemu Ya (159) : Etii.. Unadumbukia Kwenye Ulevi Na Starehe Na Ukicheche/Uplayer Ili Kumkomoa Ex Wako Mlie Break Up?? Like Real??

Tit for Tat wanaita.... kwamba ukimwaga Ugali yeye anamwaga mboga.... Watu
wengine wameanza Ulevi wa kupindukia eti kisa Break Up...mtu anaanza mapombe eti kuondoa mawazo.... Let me be very Clear here....POMBE HAIONDOI MAWAZO..... Narudia! POMBE HAIONDOI MAWAZO NA HAISAHAULISHI CHOCHOTE!

Utakunywa, utalewa tilalila, Utaamka ukiwa yuleyule! Na ukipata Marafiki wapuuzi wasio na msaada wanakusapoti kwamba kula bata, this is ur time... Jamaa alikuwa anakubana sanaaaa,hata outing ulikuwa hutoki yeeaaahhhhh we are divaaasss let us show him... SHOW WHO STUPID???

Unamshow nani... Hela utamaliza za kwako... Mwili unaounywesha Mipombe ni wa kwako.... Na Kidney Failure na Kisukari utaumwa WEWE... Dont show anyone.. Use ur brain.Usiingie kwenye Ulevi na Umalaya kisa UMEACHIKA, huo ni ujinga uliotukuka!

Wewe sio wa kwanza,mamako mwenyewe alishapigwa vibuti 88 kabla ya kuolewa na babako,muulize atakwambia.... Break Up sio mwisho wa Maisha.. Ni challenge ambazo unapaswa uzishinde na Ukiweza utajikuta umejifunza mengi sana in life.

Wale Ma-Player, sijui ni VCD Player au DVD, poleni sana... Eti unaamua kuwa Player kisa Diana amekuacha.. oh nilimpenda sana, Maisha hayana maana ngoja niwe Player.... SAWA! Kuwa Player na UKIMWI utakuwa Kocha wako.

Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Ili Kupata Posts Zangu Kirahisi Zaidi Kwenye Simu Yako.http://www62.zippyshare.com/d/FvrvpQQg/31722/xxlbongotz.apk
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies 
WhatsApp +255 715 758 021

1 comment:

  1. Ushuhuda

    Nilivunjika kabisa uhusiano wangu ulipoisha. Niliamini kweli nimepoteza upendo wa maisha yangu milele. Kisha nikampata Dk. Dawn, na kila kitu kilibadilika.
    Kwa fadhili, hekima, na mwongozo wenye nguvu, alinirudishia upendo ambao nilifikiri umetoweka. Leo, tuna furaha zaidi kuliko hapo awali!
    Dr. Dawn kweli aligeuza machozi yangu kuwa furaha.

    Dk. Dawn Anaweza Kukusaidia Na:

    ✅ Maneno ya mapenzi
    ✅ Tahadhari za Ujauzito
    ✅ Kurejesha Ndoa/Mahusiano
    ✅ Dawa za mitishamba kwa VVU, Ugonjwa wa Figo, Magonjwa ya Moyo, Maambukizi na mengine mengi.

    📧 Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
    📞 Simu/WhatsApp: +2349046229159

    Usiteseke kimya kimya. Dk. Dawn anaweza kurudisha furaha katika maisha yako!

    ReplyDelete